TRA

TRA

Saturday, June 10, 2017

Marekani yazitaka nchi za kiarabu kulegeza kamba dhidi ya Qatar

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



 
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson anasema kuwa nchi za Ghuba ni lazima ziligeze hatua yao dhidi ya Qatar ambayo inalaumiwa na majirani zake kwa kuunga mkono Ugaidi.

 Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar

Saudi Arabia, Muungano wa nchi za kiarabu, Misri na Bahrain walikata uhusiano wa usafiri na wa kidiplomasia na Qatar siku ya Jumatatu.

Bwana Tillerson anasema kuwa hatua hiyo inasabisha kuwepo madhara ya kibinadamu.

Licha la kumsifu Emir wa Qatar kwa kupuza uungwaji mkono makundi ya kigaidi, Bwana Tillerson anasema mengi yanahitaji kufanywa.
Naye Rais Trump ameishutumu Qatar kwa kufadhili ugaidi na kuitaka ikome
Awali Rais Trump alikuwa ameandika kwenye mtandao wa Twitter akiunga mkono hatua ya kuitenga Qatar, na hata kudai kuwa alishiriki katika uamuzi uliochukuliwa na Saudi Arabia pamoja na nchi zingine.
Ndege za Qatar zilipigwa marufuku ya kutumia anga za baadhi ya majirani zake.
Hatua hiyo ya ghafla ilichukuliwa baada ya msukosuko ambao umedumu miaka kadha kati ya Qatar na majirani zake wa Ghuba.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger