Majaji saba katika mahakama kuu ya maswala ya uchaguzi wameondoa kesi ambayo huenda ingepelekea rais Michel Temer, kuvuliwa mamlaka kufuatia madai ya ufisadi wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2014.
Mahakama ilichunguza ikiwa kampeni ya Roussef na Temmer mwaka 2014 ilitumia pesa ilizopata kwa njia haramu.
Iwapo rais Temer angepatikana na hatia, basi bunge la Congress lingechagua rais mpya.
Mahakama ilichunguza ikiwa kampeni ya Roussef na Temmer mwaka 2014 ilitumia pesa ilizopata kwa njia haramu.
Kesi hiyo ilifaa kuamuliwa katika kipindi cha siku tatu, japo muda uliongezwa hadi wiki moja, kutoa muda zaidi kwa majaji kuamua.
Hatimaye, umauzi wa majaji wanne kwa watatu, ulizuia bwana Temer kuvuliwa maamlaka.
Kesi ya bwana Temer ilipata mshiko zaidi, baada ya majaji kuondoa ushahidi kwamba wakurugenzi wa sekta ya ujenzi walitoa ufadhili wa mamilioni ya dola kwa uchaguzi wa mwaka 2014.
Wapinzani wa rais Temer walikuwa na matumaini kwamba uamuzi wa mahakama ungepelekea kutimuliwa kwake.
Kwa sasa anaweza akapumua, japo bado anachunguzwa kwa kupokea hongo na kuzuia haki.
SHARE
No comments:
Post a Comment