Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyabiashara katika maduka ya simu barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwa kwenye moja ya maduka ya simu eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akimsikiliza mmoja wa wakazi wa Dodoma wakati alipotembelea maeneo mbalimbali ya mji.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na mmoja wa walinzi katika eneo la barabara ya sita.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akiwasikiliza wafanyabiashara ndogo ndogo(machinga) katika eneo la ‘One way’.
Mbunge wa Dodoma mjini, Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi katika maeneo aliyotembelea.
…………………………………………………………………………..
MBUNGE wa Jimbo la Dodoma mjini,
Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya kutembelea maeneo ya katikati ya
mji na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi hasa wafanyabiashara
ndogo ndogo.
Hatua hiyo ya Mavunde imetokana
na Ofisi yake ya Mbunge kuweka utaratibu wa kuwasikiliza wananchi kero
zao na matatizo yao kila Alhamis(kero za Ardhi) na Ijumaa(Mambo ya
kijamii).
Hata hivyo kwa siku ya leo
kutokana na mapumziko ya Sikukuu ya Eid El Fitr, Mavunde ambaye ni Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu ameamua kutembea maeneo mbalimbali ya mjini
katikati na kusikiliza kero za wananchi.
Maeneo aliyotembelea ni pamoja
na eneo la ‘One way’ ambalo kuna wafanyabiashara wengi wakubwa na wadogo
na barabara ya sita ambako ni maarufu kwa maduka ya simu katika kata ya
Madukani.
Akizungumza mara baada ya
kuwatembelea wananchi hao, Mavunde ameahidi kuzipatia ufumbuzi baadhi ya
kero zinazowasibu wafanyabiashara hao.
SHARE
No comments:
Post a Comment