Matukio mbaljmbali zikionyesha
matukio wakati wa ugawaji Viuadudu vya kutokomeza Mbu wa Malaria Mjini
kibaha.Pichani ni Waziri Ummy Mwalimu akigawa Viuadudu hivyo kwa
Halmashauri kumi na moja
Na. Catherine Sungura na Benson Mwaisaka,WAMJW- Kibaha
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amempongeza na kumshukuru
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kuongeza chachu katika mapambano dhidi ya malaria kwa kununua lita
laki moja na kusambazwa kote nchini.
Ameyasema hayo wakati wa ugawaji
wa Viuadudu vya kutokomeza mbu wa malaria kwa halmashauri kumi na moja
zilizofika katika kiwanda cha kuzalisha Viuadudu hivyo kilichpo Mjini
Kibaha
Aidha ,Waziri Ummy alisema
anamshukuru Mhe. Rais kwa kumruhusu kuanza zoezi hilo kwa awamu ambapo
kwa awamu ya kwanza Viuadudu hivyo vitagawiwa kwa Halmashuri 14 nchini
ambazo zina viwango vikubwa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria,“hii
ametupa nguvu na ari sisi tuliopo kwenye dhamana ya kusimamia sekta ya
afya katika kupambana na Malaria.
Hata hivyo alisema kwa mujibu wa
takwimu toka ofisi ya Takwimu nchini zinaonyesha kwamba kiwango cha
maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini ni asilimia 14 ambapo katika
kila watoto walio chini ya miaka mitano kati ya watoto 100 watoto 14
wamekutwa na maambukizi ya Malaria
“Maelekezo yangu hasa kwa Waganga
Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni kuhakikisha dawa hii mnapulizia kuzingatia
miongozo iliyotolewa na Wizara ya Afya,Muangalie ukubwa wa eneo la
mazalia ya mbu,na kiasi kinachotakiwa kupulizia”.
Waziri Ummy amewataka wahakikishe
wanapulizia Viuadudu hivyo angalau mara nne kwa mwezi kwa maana kila
baada ya siku saba,hivyo ni lazima wanunue vifaa vya kupulizia dawa hii
pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi watakaenda kufanya zoezi hilo.
Pamoja na hayo Waziri Ummy
aliwataka ifikapo mwisho wa mwezi huu kila Mkurugenzi wa Halmshauri awe
ampelekee mahitaji halisi ili kuona ni jinsi gani watatekeleza kazi hiyo
“Lazima nipate mahitaji halisi toka Halmashauri kwa kuwa Mhe. Rais
ameshatuonyesha njia na ametuelekeza badala ya kununua dawa pia tununue
na viuadudu hivi”
Naye Mkurugenzi Msaidi toka
Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhandisi Elli Pallangyo alisema
leo hii Halmashauri kumi na moja sawa na Mikoa sita ndizo zilizofika
katika uzinduzi huo wa ugawaji wa Viuaduddu kwa awamu ya
kwanza,alizitaka Halmashauri hizo na mgawanyo wa lita kwenye mabano
Liwale(1,200), Tarime (384),
Misungwi(1,296), Kasulu(540), Songea(816),Kakonko(660), Kisarawe(720),
Kyerwa(1,080), Rufiji(5,088), Geita(2,100), Kilombero(1,140)
SHARE
No comments:
Post a Comment