TRA

TRA

Saturday, June 10, 2017

Messi aapa kusalia Barcelona hadi tamati

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


      Lionel Messi

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amesema angependa kusalia na klabu yake kwa siku zilizosalia katika taaluma yake. 

''Ni kitu ambacho nimekuwa nikikitazamia na ni kitu nilichokuwa nikikitaka," alisema. 

Kiungo huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, akashiriki mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na amefunga zaidi ya magoli 500 akiwa na klabu hiyo.

Messi ameshinda taji La liga mara nane, Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara nne na tuzo mchezaji bora duniani Ballon d'Or mara tano.
Msimu uliopita chini ya kocha Luis Enrique, Barcelona walikuwa katika nafasi ya pili kwa ligi ya La Liga, alama tatu chini ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Real Madrid.

Walishindwa 3-0 katika robo fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Juventus. 

Enrique alitangaza mwezi Machi, kwamba angeiaga klabu hiyo baada ya mkataba wake wa miaka mitatu kumalizika, mechi yake ya mwisho ilikuwa ni pale Barca walipojinyakulia kombe la Copa Del Rey . 

Messi alifunga bao la ufunguzi walipoichapa Alaves mabao 3-0 na kupata ushindi. 

Messi ambaye alikuwa wa pili nyuma ya mshambuliaji wa Real, Cristiano Ronaldo katika tuzo ya Ballon d'Or, aliuambia mtandao wa Barcelona lengo lake ni ''kujaribu kuimarika kila msimu hadi mwisho, na hilo ndilo lengo langu la msimu ujao.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger