MASERU- MKE wa Waziri Mkuu mteule
nchini, Tom Thabane (pichani katikati), ameuawa kwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ikiwa
ni siku mbili kabla ya sherehe za uapishaji kufanyika.
Mwanamke huyo, Lipolelo Thabane
anadaiwa kuuawa akiwa njiani kuelekea nyumbani pamoja na rafiki yake jana
jioni, baada ya mshambuliaji huyo mwenye silaha kuwashambulia kwa risasi.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi nchini,
Clifford Molefe, mauaji hayo yalitokea katika kijiji cha Ha Masana kilichopo
umbali wa kilometa 35 kutoka mjini hapa.
Kwa upande wake, Thabane alisema kuwa
mauaji hayo yamemsikitisha na yamemsababishia hofu kubwa.
DW
SHARE
No comments:
Post a Comment