Afisa
Muuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Cesilia Meela akiwatoa
damu baadhi ya Wakazi wa eneo la Mbagala, Jijini Dar es salaam wakati wa
zoezi la kuchangia damu lililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa
kushirikiana na Benki ya CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha
Mabasi, Mbagala Rangi Tatu, jijini Dar es Salaam jana. Jumla ya Units
106 zilipatikana.
Sehemu
ya Wakazi wa eneo la Mbagala Rangi Tatu wakishiriki zoezi la uchangiji
damu, llililofanywa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Benki
ya
CBA, iliyofanyika kwenye Kituo kikuu cha Mabasi, Mbagala Rangi Tatu,
jijini Dar es Salaam jana.
Mdau
Pina Mshana alikuwa ni mmoja wa waliochangia damu katika zoezi hilo,
ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya siku ya Damu Duniani.
Mmoja wa wachangia Damu akiingalia damu yake wakati akichangia.
Wachangia damu wakiwa kwenye foleni.
Muasisi
wa Taasisi ya Doris Mollel akijadiliana jambo na mmoja wa waauguzi
kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, wakati wa zoezi la uchangiaji
Damu, Mbala Rangi Tatu.
SHARE
No comments:
Post a Comment