Na Mathias Canal, Dar es salaam
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo June 13, 2016
amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea shule ya Msingi Hondogo iliyopo
katika Kata ya Kibamba Jijini Dar es salaam kujionea hali ya Miundombinu
ikiwemo majengo ya shule na ufanisi wa utoaji elimu katika Shule hiyo.
Mara
baada ya kuzuru katika Shule hiyo Mkurugenzi Kayombo amebaini kuwapo na
ubovu wa madarasa hivyo kuamua kujenga madarasa mengine mapya matano kwa
ajili ya wanafunzi kujisomea kwa uhuru na amani shuleni hapo.
Mkurugenzi
Kayombo alisema kuwa ujenzi huo utakaoanza hivi karibuni wa vyumba
vitano vya madarasa utaakisi pia ujenzi wa vyumba vya madarasa nane na
matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza, vivyo hivyo katika
Shule ya Msingi Kawawa na Shule ya Sekondari Mburahati ambapo kote huko
ameelekeza kuanza haraka ujenzi wa Madarasa sambamba na Vyoo kwa ajili
ya wanafunzi na walimu.
MD Kayombo alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa madarasa hayo
yatapunguza kadhia ya mbanano wa wanafunzi darasani ambapo pia amesema
ujenzi wa madarasa hayo utakuwa wa kisasa ili kukidhi mahitaji ya ubora
wa majengo ya serikali.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza jambo mara
baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo
iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto) na Afisa Uchumi
Mkuu Ndg Yamo Wambura wakikagua majengo ya shule ya msingi Hondogo
iliyopo Kata ya Kibamba wakati wa ziara ya kikazi
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza wanafunzi
kusoma kwa bidii mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule
ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua maendeleo ya
wanafunzi wa darasa la nne mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi
katika Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayomboakimsikiliza kwa makini
Mwalimu Magreth Kapinga mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika
Shule ya Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Madarasa
manne yaliyoamuliwa kuvunjwa na kujengwa upya madarasa mengine matano
katika Shule ya Msingi Hondogo Jijini Dar es salaam
Mwalimu
Happness Mashimba akiwa darasani akifundisha somo la Kiswahili darasa
la nne kwa kujitolea kipindi hiki cha likizo kama alivyokutwa na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akifurahia jambo na
wanafunzi mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya
Msingi Hondogo iliyopo Kata ya Kibamba
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa maelekezo ya kazi
mara baada ya kuzuru kwa ziara ya kikazi katika Shule ya Msingi Hondogo
iliyopo Kata ya Kibamba
SHARE
No comments:
Post a Comment