Wateja wa Vodacom Tanzania PLC ambao ni watumiaji wa huduma
ya kifedha ya M-Pesa wameanza kunufaika na gawio la shilingi bilioni
7.9.Gawio hilo limeanza kuwanufaisha jumla ya watumiaji milioni saba wa
huduma ya M-Pesa nchi nzima.
Utoaji
wa gawio unaendana na matakwa ya Benki kuu ya Tanzania. Hadi sasa
Vodacom tayari imeshatoa jumla ya shilingi bilioni 80 kama gawio ambalo
huhifadhiwa kwenye akaunti maalum ya M-Pesa Trust iliyopo kwenye benki
za biashara hapa nchini.
Kabla
ya gawio la sasa, jumla ya Tsh bilioni 72 zilishagawiwa katika awamu
tofauti tangu kampuni hii ianze utaratibu wa kutoa gawio Mwezi Disemba
2016. Utoaji wa gawio hufanyika kila baada ya miezi mitatu na gawio la
sasa ni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa biashara ya mtandao wa kampuni
hiyo, Sitoyo Lopokoiyit alisema “M-Pesa inamwezesha kila mteja kupata
huduma ya kifedha. Tunapojitahidi kumfikia kila Mtanzania, tunaendelea
kutoa huduma bora na za kisasa zinazoziwezesha Serikali na biashara
kufanya kazi pamoja na huku tukitoa faida nono kwa mawakala na wabia
wetu,” alisema
Mkurugenzi
huyo aliwaasa wateja ambao tayari wameanza kunufaika na gawio hili
kutumia fedha hizo kununua Ukarimu bando ili waweze kunufaika zaidi
kimawasiliano kwa wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na
kufanya malipo ya moja kwa moja kutoka kwenye simu zao wanaponunua
bidhaa na huduma mbali mbali na kusititiza kwamba kwa sasa kuna mamia ya
wakala wanaopokea malipo kwa njia ya M-Pesa na APP mpya ya M-Pesa
imefanya malipo kuwa rahisi zaidi.
Lopokoiyit
alifafanua kuwa, kiasi ambacho mteja anapokea kama gawio hutegemeana na
matumizi yake kupitia huduma ya M-Pesa kama kutuma pesa, kununua muda
wa maongezi, kulipa huduma na bidhaa pamoja na nyingine. Alisema Vodacom
itaendelea na jitihada za kuboresha maisha ya wateja wake kupitia
huduma mbali mbali mbali na kuwataka wateja wa Vodacom kuendelea kutumia
huduma ya M-Pesa ili waweze kunufaika na mambo mbali mbali ikiwamo
gawio.
SHARE
No comments:
Post a Comment