Otto Warmbier,
mwanafunzi mwenye asili ya Marekani aliyekuwa na umri wa miaka ishirini
na miwili, aliyerejeshwa nchini humo wiki iliyopita baada ya miezi kumi
na mitano ya kushikiliwa nchini Korea Kaskazini, amefariki dunia siku
sita tu baada ya kuachiliwa.
- Korea Kaskazini yamwachilia huru Mmarekani
- Mwanafunzi aliyeachiliwa na Korea Kaskazini alazwa hospitalini
- Korea: Tulimwachilia mwanafunzi kwa misingi ya kibinadamu
- Mmarekani aliyekamatwa Korea Kaskazini atambuliwa
Akielezea hali ya kijana huyo amesema alikuwa katika hali ya kutojitambua pindi alipoachiliwa kutoka jela , na kuanzia hapo alilazwa hospitalini kwa matibabu zaidi karibu na nyumbani kwake Cincinnati.
Madaktari waliokuwa wakimtibia kijana huyo katika hospitali ya chuo kikuu cha tiba mjini humo wamesema kwamba kijana huyo alikuwa na majeraha makubwa ya kuumia neva.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment