Ofisi ya Rais
nchini Nigeria imekiri kuwa ndege rasmi ya Rais Muhammadu Buhari
imeegeshwa kwa zaidi ya siku 50 kwenye uwanja wa ndege mjini London.
Rais Muhammadu Buhari (kushoto) na makamu wake Yemi Osinbajo
Ofisi ya Rais ilikuwa ikijibu ripoti za mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya watu nchini Nigeria, wameelezea ghadhabu yao kutokana na kuegeshea ndegr hiyo mjini London.
- Buhari: Sijawahi kuwa mgonjwa kupitia kiasi
- Aliyempa mbwa wake jina 'Buhari' ashtakiwa Nigeria
- Rais Buhari aonekana hadharani kwa mara ya kwanza
Msemaji wa Rais, Garba Shehu, alikana kuwa nchi inalipa pesa nyingi kwa nafasi hiyo. Aliiambia BBC kuwa gharama ya kuegesha ndege hiyo haitazidi pauni 1000.
Rais Buhari amekuwa nje ya nchi kwa karibu miezi miwili kupata matibabu mjini London.
SHARE
No comments:
Post a Comment