Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akizungumza muda mfupi baada ya
kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi wa mchanga wa madini (makinikia)
kwenye makontena Ikulu jijini Dar es Salaam Juni 12, 2017.
Akiongea
kwa hisia kali, Rais aliwaambia watanzania "Nimejitolea damu yangu kwa
ajili ya taifa letu, siwezi kukaa kimya huku rasilimali ambazo
tumejaaliwa na Mungu, zikiporwa tu.
"Katika ripoti hiyo ya Profesa
Nahemiah Osoro, imebaini kuwa taifa limepoteaza kiasi kinachozidi
Trilioni 300 kutokana na rasilimali zitokanazo na madini tangu mwaka
1998 kazi ya uchimbaji madini ilipoanza kwenye migodi ya Bulyanhulu
mkoani Kahama, na kufuatiwa na Buzwagi na North Mara ambayo kwa sasa
inamilikiwa na kampuni ya Acacia. Taarifa hiyo imependekeza mawaziri
wote wa zamani waliohudumu kwenye wizara ya Nishati na Madini, Mhe.
Danel Yona, Mhe. Nazir Karamagi, Mhe. William Ngeleja, makatibu wakuu wa
wizara hiyo, wanasheria wa wizara, wanasheria wakuu wa serikali
wastaafu, Andrew Chenge, na Mwanyika wahojiwe na vyombo vya ulinzi na
usalama na ikibainika walikiuka sheria wafikishwe mbele ya vyombo vya
sheria.
Hata hivyo, katika taarifa yake iliyotoa jioni ya Juni 12, 2017,
Kampuni ya Acacia imekosoa taarifa hiyo ya uchunguzi ya tume ya pili ya
Rais na kusisitiza Acacia haijavunja sheria yoyote ya nchi na imekuwa
ikifanya shughuli zake kwa mujibu wa mikataba baina yake na serikali.
Rais na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, wakipitia ripoti hiyo
Rais akimkabidhi nakala ya ripoti hiyo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa
Picha ya pamoja
Baadhi ya wageni waalikwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya Kamati ya pili ya
Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa
nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa
nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro Ikulu
jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo
kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye
machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini wakati ikifunguliwa
kwenye kabrasha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya
pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga
unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu
mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kukabidhiwa
Ripoti hiyo ya Kamati ya Pili ya Uchunguzi wa Madini Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama na Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai, Kaimu
SHARE
No comments:
Post a Comment