Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya NMB, Omary Mtiga
akizungumza na zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa
Ramadhani kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es
Salaam. NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija
Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine katika
kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika wamefanikiwa kufuturisha watoto hao
yatima kutoka vituo mbalimbali vya jijini Dar es Salaam.Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Banki ya NMB, Omary Mtiga
(wa pili kulia) akitoa zawadi kwa watoto walioshiriki katika futari
iliyoandaliwa na Mbunifu wa Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni
mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau wengine ikiwemo Benki ya NMB katika
maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Shughuli hiyo ilifanyika katika
ukumbi wa Shabaan Robert uliopo Upanga na kuhudhuriwa na wageni
mbalimbali pamoja na wadau waliosaidia kufanikisha jambo hilo wakiwemo
NMB na wengine.Baadhi
ya watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo
mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam wakiwa katika
futari iliyoandaliwa na NMB kwa kushirikiana na Mbunifu wa Mavazi
nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na wadau
wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.Sehemu ya
watoto waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani kutoka vituo
mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam, wakiwa katika
futari iliyoandaliwa na NMB (mdhamini) kwa kushirikiana na Mbunifu wa
Mavazi nchini, Khadija Mwanamboka ambaye ni mmiliki wa mgahawa wa VVK na
wadau wengine katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika..Sehemu
ya zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani
kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam
wakiwa katika futari hiyo kwenye Ukumbi wa Shaan Robert.Sehemu
ya zaidi ya watoto 450 waliopo kwenye mfungo mtukufu wa Ramadhani
kutoka vituo mbalimbali vya watoto yatima vya jijini Dar es Salaam
wakiwa katika futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwenye Ukumbi wa
Shaan Robert.
No comments:
Post a Comment