Mwalimu
wa Elimu ya Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao
Makuu Bw. Gabriel Mwangosi akielezea jambo wakati wa Mdahalo wa Vijana
kuhusu Nguvu ya Kodi, ulioandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana
Tanzania (TYVA) Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa
TYVA Taifa Bw. Suleiman Makwita na Muongoza mada Bi. Nuria Mshare. Kauli
mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Mwenyekiti
wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bw. Suleiman
Makwita akifafanua jambo wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na
asasi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Muongozaji wa
mdahalo huo Bi. Nuria Mshare na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi.
Muongozaji wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa
na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi. Nuria Mshare
akifafanua jambo wakati wa mdahalo huo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka
kulia ni Mwenyekiti
wa TYVA, Bw. Suleiman Makwita na Mwalimu wa Elimu ya Kodi kutoka
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu Bw. Gabriel Mwangosi. Kauli
mbiu ya mdahalo huo ni “Nguvu ya Kodi” Kodi kwa Huduma Bora za Jamii.
Makamu
Mwenyekiti wa Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) Bi.
Irene Kalumuna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa mdahalo hukusu kodi ulioandaliwa na asasi hiyo leo Jijini Dar
es Salaam.
Washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa
na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakichangia mada
wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi
wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya
udhamini wa Shirika la Action Aid Tanzania.

Baadhi ya washiriki wa Mdahalo wa Vijana kuhusu umuhimu wa kodi uliondaliwa
na Asasi ya Kiraia ya Dira ya Vijana Tanzania (TYVA) wakifuatilia mada
wakati wa mdahalo huo uliofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
Jijini Dar es Salaam leo. Mdahalo huo umeandaliwa na TYVA kupitia mradi
wake wa Ushiriki wa Kijana katika masuala ya Kodi (YEGA) chini ya
udhamini wa Shirika la Action Aid.(PICHA NA FRANK SHIJA – MAELEZO)
SHARE
No comments:
Post a Comment