Mkurugenzi
wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Ibrahim Mahumi akitoa
ufafanuzi kuhusu taratibu zinazohusu menejimenti ya Rasilimaliwatu
serikalini kwa viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe katika
Ofisi za Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka.
Viongozi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakizungumza masuala
ya kiutumishi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka 2017.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Bi. Amina Kiwanuka
akieleza utekelezaji wa masuala ya kiutumishi katika eneo lake la kwa
Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
waliomtembelea ofisini kwake leo alasiri kuhimiza uwajibikaji ni sehemu
ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2017.
Mkuu
wa Idara ya Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya
Wanging’ombe Bw. Abdullfariq Mkata (wa pili kulia) akitoa taarifa ya
kiutendaji ya Idara yake kwa Viongozi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma walipoitembelea Halmashauri hiyojana kuhimiza
uwajibikaji ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
kwa mwaka 2017.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma wa Ofisi ya
Rais,Menenimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Issa Ng’imba akitoa ufafanuzi
kuhusu masuala ya kiutumishi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Wanging’ombe Bi. Amina Kiwanuka ofisini kwa mkurugenzi huyo jana ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka
2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Amina
Kiwanuka akisikiliza kwa makini.
SHARE
No comments:
Post a Comment