Mkufunzi anayesimamia mafunzo ya
Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara wa Mwaka
2017/18 (2017/18 HBS) Sergiy Redyakin akimwelekeza mmoja wa washiriki wa
mafunzo hayo kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) namna ya kujaza
dodoso litakalotumika katika utafiti huo unaotarajia kufanyika nchini
kuanzia mwezi Agosti, 2017.
Baadhi ya Watakwimu wa Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS) wakifuatilia kwa makini mafunzo yanayotolewa na
mkufunzi anayesimamia mafunzo hayo Sergiy Redyakin (hayupo pichani)
wakati wa mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 yaliyofanyika hivi karibuni katika makao
makuu ya NBS Dar es Salaam.
Baadhi ya watakwimu kutoka NBS
wakijifunza namna ya kujaza madodoso kwa njia ya kieletroniki wakati wa
mafunzo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi Tanzania Bara
wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia mwezi Agosti,
2017.
Mtakwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Hellen Mtove (wa kwanza kulia) akimhoji mmoja wa wanakaya
wakati wa majaribio ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi
Tanzania Bara wa Mwaka 2017/18 unaotarajia kufanyika nchini kuanzia
mwezi Agosti, 2017.
(PICHA NA EMMANUEL GHULA)
SHARE
No comments:
Post a Comment