TRA

TRA

Wednesday, June 14, 2017

Simchukii Wema, nampenda, lakini...

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Said Mwishehe

KWA Ujunga Wangu nimekuwa nikimfuatilia kwa karibu sana huyu mwanadada mrembo na mwenye uzuri wake wa sura na sauti Wema Sepetu.

Sijui kwanini ila naona raha tu kufuatilia mambo yake.Kuna mambo mengi ambayo anayafanya wakati mwingine yananifurahisha na mengine mengi tena mengi kweli yanakera.Pamoja na kuwa baadhi ya mambo yake siyapendi lakini nashindwa kutofuatilia habari zake na hasa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Najua na wewe unafahamu kuwa Wema ni moja kati mabinti wa Kitanzania waliobahatika kukubalika ndani ya jamiii. Umaarufu wa Wema ni wa muda mrefu na hasa ni pale baada ya kuwa Miss Tanzania mwaka 2006.




Hivyo kwenye orodha ya waliowahi kuwa Ma-Miss Tanzania kwenye nchi yetu Wema naye yumo.Kwa maana hiyo ni mrembo ambaye umaarufu wake upo katika kila kona.

Pia uwezo wake katika tasnia ya uigizaji nayo ikamfanya kuongeza idadi ya watu wanamfahamu. Wema anajulikana sana na kama kuna watu hawamfahamu basi ni wachache.

Natambua kwa ukubwa wa nchi yetu na watu wake huenda kuna baadhi ya maeneo hawamfahamu Wema.

Si jambo la kushangaza sana kwani wapo baadhi ya watu hata kwenye mtaa wako unaokaa hakuna anayewajua zaidi ya familia yake na nyumba moja au mbili ya majirani yake. Itoshe kusema Wema ni maarufu na tangu mwaka 2006 hadi leo hii ameendelea kuwa maarufu.





Kwa Ujinga Wangu nimekuwa nikivutiwa sana na Wema kutokana na namna ambavyo anaigiza kwenye filamu mbalimbali. Kuna wakati natamani filamu yote awe anaonekana kila nukta ya sekunda na ikiwezekana kila dakika.

Ila utengenezaji wa filamu haupo hivyo, unatoa nafasi kulingana na namna ambavyo mhusika anacheza. Wapo wanaonekana mara moja tu katika filamu ya dakika 70.

Kwa Wema anayo bahati maana wengi wanaomshikirisha kwenye filamu zao wanampa muda wa kutosha na kuonekana zaidi ya wengine. Ukitaka kuamini angalia filamu ya 'Four Teen Days'

Kwa kuwa Wema ni binti ambaye anatamani kujaribu kufanya mambo mengi, mbali ya kuigiza filamu za kibongo, pia amekuwa akifanya mambo mbalimbali yanayohusiana na harakati za siasa na mambo mengine kwenye jamii.

Katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 aliamua kujitosa kuwania ubunge wa Viti Maalum kupitia Mkoa wa Singida kwa tiketi ya CCM lakini akaanguka kwenye kura za maoni. Haikuwa bahati yake.



Kuikosa nafasi hiyo haikumfanya awe kando kwenye uchaguzi huo kwani alianzisha kundi la Mama ongea na mwanao ambalo lilisheheni waigizaji wa filamu maarufu nchini na kisha wakazunguka nchi zima kumuombea kura aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Magufuli ambaye kwa sasa ndio Rais wetu mpendwa.

Wema na kundi lake walijikita zaidi kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu wakati huo wa mchakato wa uchaguzi mkuu. Hivyo wasiomfahamu Wema kama Miss Tanzania mwaka 2006, wasiomfahamu Wema kama muigizaji filamu sasa wakamfahamu kama moja ya waigizaji maarufu nchini waliokuwa wakiwaombea kura wagombea wa CCM.

Kwa Ujinga Wangu mtu wa aina hii lazima niwe karibu kufuatilia kila ambacho anakifanya. Niseme tu bila kupoteza muda pamoja na kufurahishwa na juhudi za Wema katika shughuli zake za kila siku, amekuwa akinikera kwa tabia yake ya kuitumia mitandao ya kijamii vibaya.

Nasema hivyo kwasababu kuna baadhi ya mambo ambayo huwezi amini kama mtu anayejitambua anaweza kuweka lakini ghafla utakuta mambo yapo mtandaoni.

Sitaki kuzungumzia hili la sauti yake iliyosamnbaa kwenye mitandao ya  kijamii akiwa na moja ya wanasiasa maarufu nchini. Sitaki kuizungumzia hiyo kwasababu huenda si sauti yake ingawa nasikia amekiri ni yake na wengine kusema ameikana.

Natambua Wema ni moja kati ya warembo ambao wanapenda kuweka mambo yao kwenye mitandao lakini ni vema akawa na uchaguzi sahihi kipe aweka na kipi kibaki kwenye simu yake. Kwa Ujinga Wangu hata hili la Sauti yake akiwa na huyo kigogo wa siasa ilipaswa kubaki kwenye simu yake.

Ninaposema Wema anakera basi ni hili eneo la mitandao ya kijamii. Ieleweke simchukii Wema, nampenda lakini hili la kwenye mitandao ya kijamii sipendezwi nalo. Wakati wengine wakiitumia mitandao ya kijamii katika kufanikisha ndoto zao za kimaisha na kujijengea heshima kwenye jamii yeye anaitumia mitandao hiyo kuiboa heshima yake ambayo naamini ameijenga kwa muda mrefu.

Nimpongeze Wema kwenye magazeti ya udaku siku hizi  haonekani sana , nadhani ni kwasababu sasa ameamua kuhamia kwenye mitandao ya kijamii kufanya yake. Kupitia mitandao ya kijamii Wema alijikuta akitofautiana na rafiki yake wa siku nyingi  wake Stive Nyerere.

Sitaki kuelezea namna ambavyo ilivyokuwa maana wote tunakumbuka.Wema akaamua kumtikia Chadema lakini haijapita hata mwaka tayari huko nako kaharibu tayari.

Wema tambua thamani yako katika jamii na kisha pima kila jambo ambalo unataka kulifanya. Halafu angalia faida na hasara.Hiyo itakusaidia kupita katika njia sahihi. Nikiri nimekuwa mtumwa wa kufuatilia kila unachokifanya.Nitumie nafasi hii kama utanisoma nakwambia hivi Dada Wema jirekebishe.

Nyota yako bado inang'ara, usikubali ififie kwa mambo yasiyo na tija. Achilia mbali kutofautiana na Stive Nyerere kwasababu tu ya mambo hayo hayo ya simu na mitandao, nakumbuka hata uhusiano wako wa kimapenzi na 'Modo'

Kalisa nao ulifika tamani baada ya mambo ya chumbani nayo kuyaweka kwenye mitandao ya kijamii.

Najua ulikataa kuwa haukuisambaza wewe na mwenzio naye alikataa.Ila simu iliyotumika kurekodi ilikuwa yako. Hili si jambo jema kwako.Ndoto zako kwenye maisha zitafanikiwa iwapo utakuwa makini kwa kila unachokifanya.

Kwa Ujinga Wangu natamani kukuona Wema ukipumzika kwa muda kuitumia mitandao ya kijamii ili kulinda heshima yako.

0713833822


Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger