Msanii
Kayumba kutoka Mkubwa na Wanawe ambaye pia ni mshindi wa shindano la
BSS 2015, amefunguka sababu zinazomfanya asitumie jina lake vibaya.
Fid
Q amewahi kurap kwenye wimbo wake ‘Agosti 13’ kuwa “Ustaa ni mzigo wa
mwiba, ukiubeba utaumia.” Kupitia kipindi cha Zero Planet cha Ice FM ya
Njombe, muimbaji huyo amesema msanii ni kioo cha jamii na kila kitu
ukifanya jambo baya heshima yako inapungua.
“Msanii
ni kioo, kwa hiyo mimi nikifanya jambo la ajabu linaweza kunishusha.
Kwa hiyo heshima pia inapungua, so msanii ni heshima na msanii ni kioo.
Msanii ni kila kitu,” ameongeza kuweka mkazo katika tofauti ya watu hao
wawili.
Kayumba kwa sasa ameachia ngoma mpya aliyomshirikisha Aslay inaitwa ‘Mtoto Mbichi’.
SHARE
No comments:
Post a Comment