MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imejivunia kujenga shule ya kisasa
ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba Mjini
ili iwe mbadala wa shule ya Tumaini iliyopo eneo la karibu na uzio wa
Kiwanja cha ndege.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Salim Msangi amesema shule hiyo inamajengo
tisa yenye madarasa 24 kati ya hayo 21 ni ya watoto wasio na mahitaji
maalum na matatu ni ya watoto wenye mahitaji maalum; zipo ofisi za
walimu, vyoo vya shule na vya walimu, na nyumba ya kukaa mwalimu mmoja.
“Ninaona
fahari kubwa na nimefarijika sana kuona shule imekamilika kwa kiwango
kikubwa na sasa watoto wetu watasoma katika mazingira ya ya utulivu na
amani tofauti na awali katika shule ya Tumaini kulikuwa na kelele za
ndege kila zinapotua na zinaporuka,” amesema bw. Msangi.
Pia
Bw. Msangi amesema shule ya zamani ilikuwa katika maeneo hatarishi ya
karibu na barabara ya kutua na kuruka kwa ndege, jambo ambalo lingeweza
kuleta maafa makubwa endapo kungetokea ajali maeneo hayo.
Naye
mkandarasi wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi ya CMG ya Mwanza,
Mhandisi Jumanne Warema amesema pia madarasa hayo yatawekewa madawadi
315, meza na viti 16 za walimu na madarasa ya watoto wenye mahitaji
yatawekwa viti maalumu 48.
Mkuu
wa shule ya Tumaini, Theophil Ndyakowa ameishukuru TAA kwa msaada
huo mkubwa walioutoa kwa ujenzi wa shule ya kisasa, ambapo sasa
wanafunzi watasoma kwa bidii zaidi.
Hata
hivyo mradi huo wa shule umedhaminiwa na Benki ya Dunia, ambapo pia
wamefanikisha ujenzi wa jengo la kisasa la abiria, jengo la kuhifadhi
umeme na kukarabati barabara ya kutua na kuruka kwa ndege.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi),
Dr. Leonard Chamuriho (watatu kushoto) akiwafafanulia jambo wahandisi
Diana Munubi na Mbila Mdemu (kushoto) huku Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi (mwenye
suti nyeusi) akisikiliza mara baada ya kukagua shule mpya ya msingi ya
kisasa ya Tumaini iliyopo Bukoba.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa shule
ya kisasa ya msingi ya Tumaini iliyopo kata ya Mafumbo, wilaya ya Bukoba
Mjini.
Wanafunzi
waliohamishiwa kutoka katika shule ya msingi Tumaini iliyokuwa maeneo
ya karibu na kiwanja cha ndege cha Bukoba, sasa wakiwa mapumziko kwenye
shule mpya iliyojengwa maeneo ya Mafumbo kwa usimamizi wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA
Wajumbe
wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB),
wakiwa nje ya madarasa ya shule mpya ya kisasa ya msingi ya Tumaini
baada ya kufanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB),
Prof. Ninatubu Lema (aliyevaa fulana nyeupe mbele), na wajumbe wengine
wakimsikiliza mmoja wa walimu wa shule hiyo wakiwa ndani ya ofisi ya
walimu wa shule hiyo.
Shule
ya zamani ya msingi ya Tumaini iliyo karibu na eneo la kiwanja cha
Ndege Bukoba na sasa imehamishiwa mbali eneo la Mafumbo kutokana na
usalama.
SHARE
No comments:
Post a Comment