NA MWANDISHI WETU
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) inafanya ziara ya siku tatu
nchini Israel kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini hasa
wanyamapori wanaopedwana raia wa nchi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar
es Salaam juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Devota Mdachi alisema ziara
hiyo itakayoanza Juni 11 hadi 15 mwaka huu itawasaidia kukutana na wadau
mbalimbali wa sekta ya utalii ikiwemo vyombo vya habari na wawekezaji.
“Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii pia atakuwa
sehemu ya ziara hii, ambapo tutakutana na wadau zaidi ya 100 wa utalii pamoja
na mawakala wa utalii tutakaowashawishi watuletee watalii wengi zaidi.
“Takwimu zinaonyesha kila mwaka watalii kutoka Israel
wanaongezeka, kwa mfanoo mwaka 2011 walikuja watalii 3000 kutoka Israel na
mwaka 2016 walikuja 15,000 ni 0ngezeko la zaidi ya mara tano ndani ya miaka minne,”
alisema Bi. Devota.
Aliweka wazi kuwa watakapokutana na wenyeji wao Bodi ya
Utalii Israel watakuwa na mazungumzo ya kina kuhusiana na kubadilishana uzoefu
katika sekta hii muhimu kwa maendeleo ya nchi pamoja na kujua mbinu wanazotumia
kupata watalii wengi.
“Tunajua Israel ni taifa la kiroho, historia yake
inajipambanua kuwavutia watua wengi kuitembelea, lakini hata sisi nchini kwetu
kuna maeneo mengi ya kihistoria tutahakikisha tunayatangaza kadiri
tutakavyoweza, kwa sababu sehemu ya ziara yetu tutazungumza katika redio
mbalimbali za nchi hiyo ikiwemo redio ya taifa inayosikika Israel nzima.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Taifa ya Utalii (TTB) Bi. Devotha Mdachi(kulia) akimwelekeza
Balozi wa ukarimu 'Goodwill Ambassador' wa TTB Irene Veda sehemu za
kusaini mkataba wake wa miaka miwili hivi karibuni.
“Hivi tunavyozungumza tayari matangazo katika redio
yanaendelea kuwa kuna ujumbe unatoka Tanzania kuja kutangaza vivutio vya
utalii, Waisrael kila mwaka wanakuja kuangalia mbuga za wanyama tunajua
wanapenda sana wanyamapori,” alisema Bi. Devota.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo wa TTB alibainisha
kuwa katika ziara yao watakuwa na siku moja ya kukutana na wawekezaji upande wa
malazi, yaani hoteli.
Ambao watawashawishi waje kuwekeza nchini ili ongezeko la
watalii liendane na malazi bora yenye hadhi ya kimataifa.
Tanzania ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kuwa na
vivutio vingi vya kitalii, inakadiriwa zaidi ya asilimia 38 ya ardhi yake
imehifdhiwa kwa ajili ya utalii.
Vilevile sekta hii inachangia asilimia 13 ya
pato la taifa, mwaka 2013 iliingizia taifa pato la Dola za Kimarekani bilioni 4.48
zawa na zaidi ya Sh trilioni tisa.
Mwisho
SHARE
No comments:
Post a Comment