Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla
pamoja na Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Taifa Joheli Festo wakiangalia
ripoti iliyozinduliwa leo na shirika Save the Children kuhusu hali ya
ndoa za ututoni duniani wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika
liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla
akihutubia wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika
leo katika mji wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akihutubia
wajumbe wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika
mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla
akipata Maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi masuala ya Watoto wa
Wizara yake kuhusu kazi za Wiazara wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto
wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla
akipata Maelekezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi masuala ya Watoto wa
Wizara yake kuhusu kazi za Wizara wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto
wa Afrika liliofanyika leo katika mji wa Dodoma.
Mkuu wa idara ya ulinzi na haki
za mtoto wa shirika la Plan International Tanzania, Jane Mrema
akiwasilisha taarifa ya matokeo ya tafiti za ndoa za utotoni wakati w
wakati wa Kongamano la Siku ya Mtoto wa Afrika liliofanyika leo katika
mji wa Dodoma.
…………………………………………………………………..
NA ANTHONY ISHENGOMA
Wasichana Nchini Tanzania
wanakumbana na changamoto mbalimbali katika makuzi yao ikiwemo ukatili
wa kingono hususani mimba za utotoni kabla ya kufikia miaka 18.
Akiongea na vyombo vya habari
mjini Dodoma leo katika Kongamano la maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Afrika Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Hamis Kigwangala amesema takwimu zinaonesha kuwa asilimia
51.4 ya idadi ya watoto ni wasichana pia takwimu zinaonesha kuwa mtoto
wa kike 1 kati ya 3 na wa kiume 1 kati ya 7 anakumbana na ukatili wa
kingono kabla ya kufikia umri wa miaka 18.
Mhe. Kigwangala aidha amesema
kuwa takwimu zinaonyesha kuwa uwiano wa wasichana na wavulana katika
elimu ya msingi na sekondari ni uwiano wa moja kwa moja (1:1), ingawa
idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto wanazokutana nazo
ikiwa ni pamoja na mimba na ndoa za utotoni.
‘’ Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu
kwa Mwaka 2012 hadi 2016 idadi ya watoto wa kike walioacha shule
kutokana na kupata ujauzito ni 610 (mwaka 2011), 2,433 (mwaka 2012),
247 (mwaka 2013), 265 (mwaka 2014 na 251 (mwaka 2015). Serikali
inaendelea kukabiliana na changamoto hizi ili kuhakikisha wanafunzi wa
kike wanapata elimu hadi kufikia ngazi ya vyuo alisema Mhe.
Kigwangala’’.
Ametaja madhumuni ya kuadhimisha
siku hii kuwa ni kutoa fursa kwa wazazi, walezi na wadau wote wa haki
za mtoto kutafakari changamoto zinazowakabili kama vile ukatili katika
Bara letu la Afrika kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi.
Maadhimisho ya siku hii hapa
Nchini hutumika kutathmini changamoto zinazowakabili watoto katika
upatikanaji wa haki, malezi, elimu, afya na ulinzi kwa lengo la
kuboresha huduma hizi ili ziweze kumfikia kila Mtoto nchini.
Aidha amesema siku siku hii
inatumika kuwakumbusha na kuwahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla
kuzingatia jukumu lao la msingi la utoaji haki na huduma za ustawi wa
Mtoto bila ubaguzi wowote. Siku hii hutumika kufanya ushawishi kwa wadau
kuwekeza katika maeneo ya malezi, afya, elimu, ulinzi kwa lengo la
kuunga mkono jitihada za Serikali za kumwendeleza Mtoto.
Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa
Afrika yametokana na Azimio lililopitishwa na iliyokuwa Jumuiya ya Nchi
Huru za Umoja wa Afrika (OAU) kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa
shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto, nchini Afrika ya
Kusini tarehe 16 Juni 1976.
Aidha Katika tukio hilo la
kusikitisha, inakadiriwa kuwa takribani watoto 700 waliuawa kikatili
wakiwa kwenye harakati za kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi iliyokuwa
inataolewa na serikali ya makaburu.
SHARE
No comments:
Post a Comment