TRA

TRA

Tuesday, June 20, 2017

Unafahamu umuhimu wa TUCO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Mwandishi Wetu

UMEWAHI kujiuliza kwa nini waajiri wengi hawapendi kuwa na vyama vya wafanyakazi maeneo ya kazi?

Jibu lake ni dogo tu. Ni kwa sababu wafanyakazi watapata mahali pa kuzungumzia changamoto zinazowakabili, ikiwepo kutopewa mikataba au mazingira bora ya kazi.

Pamoja na kuwepo kwa hali hiyo, Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda na Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) hakijabaki nyuma kutimiza majukumu yake.

 



Katibu Mkuu wa TUICO, Boniface Nkakatisi (kushoto) akisaini mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi na Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group, Roberto Jarrin (kulia) katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama siku za hivi karibuni.
 

Chama hicho kimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha maeneo ya kazi kunakuwa na matawi na viongozi ambao watahakikisha haki za wafanyakazi zinazingatiwa.

Kumbukumbu zinaonesha TUICO imeshiriki mara nyingi kutatua migogoro mingi maeneo ya kazi, kama ambavyo kimewahi kufanya kiwanda cha urafiki.

Ukizungumza na Katibu Mkuu wa TUICO, Boniface Nkakatisi atakwambia namna kimefanya kazi kubwa kutetea wafanyakazi katika maeneo yao.

Kokote anakopita kwa shughuli za utendaji amekuwa akisisitiza upendo ili watu waweze kufanyakazi kwa tija. Ikumbukwe kuwa TUICO ipo  kutetea maslahi ya mwajiri na mwajiriwa. 

Ieleweke kuwa TUICO ina majukumu mengi kuanzia kwenye viwanda, biashara na taasisi za fedha hivyo wafanyakazi wahakikishe wanajiunga nacho maeneo yao ya kazi.

Lengo kubwa ni ili kiweze kupigania maslahi yao pamoja na waajiri pale inapotokea mvutano kati yao na uongozi.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger