TRA

TRA

Wednesday, June 28, 2017

Viongozi wawili wa serikali wadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi Kibiti

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 
Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Aidha, Kamanda wa Polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi.

Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger