Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii
Kanda ya Kaskazini.
Wachezaji
30 wa timu za soka za mataifa mbalimbali wameshiriki kuweka rekodi ya
kwanza Duniani kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika mlima Kilimanjaro
,umbali mita 5731 kutoka usawa wa bahari.
Rekodi
nyingine iliyowekwa ni ile ya mwamuzi wa kike wa Tanzania
anayetambulika na Shirikiho la Soka Duniani (FIFA) Jonesia Rukyaa
kuchezesha mchezo huo wa dakika 90 uliomalizika kwa sare ya bila
kufungana .
Kundi
la Wanamichezo 60 wakiwemo wachezaji 30 wa timu za taifa za wanawake
kutoka mataifa zaidi ya 20 walioshiriki kuweka rekodi ya kucheza soka
katika eneo la kreta lililopo katika kilele cha Uhuru.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki mchezo wa soka katika Kilele cha uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) Betrta Loibook
akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini ,Devota Mdachi
walipowapokea wachezaji wa timu za taifa za wanawake wakati wakishuka
kutoka Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Mwika.
Mhifadhi
Mkuu KINAPA,Betrita Loibook pamoja na Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya
Utalii,Geofrey Tengeneza wakifurahia mara baada ya wachezaji wa timu za
taifa za wanawake kutoka mataifa mbalimbali duniani kuweka rekodi ya
kucheza mpira katika kilele cha Uhuru .
Wachezaji
wa timu za Taifa wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa
Bodi ya utalii pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Timu za Gracier fc na Volcano fc zikijiandaa kwa mchezo wa kirafiki katika eneo la Kreta,kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro.
Wachezaji wakiweka pozi la picha katika Kreta ya Uhuru katika kilele cha Uhuru juu ya Mlima Kilimanjaro.
SHARE
No comments:
Post a Comment