
Na Mwamvua Mwinyi ,Kibiti
Watu watatu wakazi wa
kijiji cha Nyamisati, wilayani Kibiti wanadaiwa kufariki dunia kwa
kupigwa risasi usiku wa kuamkia Juni 9 na watu wasiojulikana.
Ndani ya siku saba watu
wanne wamekufa kwa kupigwa risasi Kibiti na Rufiji, mmoja amenusurika
kifo kwa kupigwa risasi ya kichwa na mmoja ametekwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema miongoni kwa watu waliouwawa yupo mwenyekiti wa kitongoji Moshi Machela.
Kwa mujibu wa mashuhuda hao watu waliouawa ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gulamuhusein Kifu alithibitisha kutokea kwa tukio hili Juni 8 mwaka huu .
Alisema kwamba amepokea
taarifa ya kutokea kwa mauaji hayo na hivyo bado hana taarifa zaidi
licha ya kumuagiza OCD kwenda eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi .
“Lakini jeshi na askari
polisi bado wapo kazini wakiwasaka wahalifu hawa wanaoendelea kumaliza
watu wasio na hatia ,” alisema Kifu .
Mnamo Juni 7 majira ya
saa 7, Nurdin Mohammed Kisinga alijeruhiwa baada ya kupigwa risasi ya
kichwa ,na watu wasiojulikana huko kijiji cha Ngomboroni kata ya Umwe
Kaskazini,Ikwiriri wilayani Rufiji.
Hata hivyo ,mkazi mwingine,Eric Mwarabu ambae alikuwa ni askari mgambo alifariki mara baada ya kupigwa risasi nyumbani kwake.
Pia maiti ya mwanaume
ambae hajajulikana jina iliokotwa mchana june 7 huko kijiji cha Mtunda
A,kitongoji cha Ngwaro,kata ya Mtunda wilaya ya Kibiti.
Katibu wa CCM kata ya Mtunda, Abdallah Mayonjo alieleza,maiti hiyo
iliokotwa ikiwa imefungwa kamba mikononi na miguuni.
Mbali ya hayo ,mtu mwingine ameokotwa akiwa amefariki dunia kijiji cha Kipoka ,Ikwiriri wilayani Rufiji huku ikiwa haina nguo.
SHARE
No comments:
Post a Comment