TRA

TRA

Friday, June 23, 2017

Watu watatu wauawa Mandera

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Polisi nchini Kenya wanasema washambuliaji wamewapiga risasi na kuwaua watu watatu wakati wa uvamizi wa benki moja ya kibiashara kaskazini mashariki mwa nchi hiyo hivi leo.
Waliouawa ni raia wawili na afisa mmoja wa polisi katika mashambulizi hayo kwenye Kaunti ya Mandera, kwa mujibu wa kamanda wa polisi, Charles Chacha.

"Kulikuwa na majambazi watano wenye silaha. Walipofika kwenye benki, walimpiga risasi afisa wa polisi aliyekuwapo mlangoni, na polisi walifanikiwa kumpiga risasi mmoja wa wahalifu hao, lakini...walikimbia," Chacha aliliambia shirika la habari la Reuters.

Elwak, mahala hasa ambapo mashambulizi hayo yametokea, pako karibu na mpaka wa Somalia.

Shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu linasema pia kuwa bomu lililotegwa barabarani limeripuka kwenye mji huo huo wa Mandera, ingawa hakuna taarifa za waliouawa ama kujeruhiwa kwenye mripuko huo.

Mandera imekuwa ikishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara, ambayo yameangamiza maisha ya maafisa kadhaa wa usalama na raia wa kawaida. 

Kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaida limekuwa likibeba dhamana ya mashambulizi hayo.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger