Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu kambi maalum ya
matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi hiyo kwa kushirikiana na Taasisi
ya Madaktari Afrika ya nchini Marekani kwa wagonjwa ambao mapigo yao ya
moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum cha kurekebisha
mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) . Kushoto ni
Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Mathew Sackett. Tangu kuanza kwa
kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20 wameshapatiwa
matibabu kati ya hao nane wamewekewa Pacemaker na wengine wanne
wanatarajia kuwekewa leo na kesho.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini
Marekani Mathew Sackett akizungumza na waandishi wa habari na
kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa ulioufanya katika matibabu ya
Moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayofanywa na Taasisi
hiyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa wagonjwa
ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa kifaa maalum
cha kurekebisha mapigo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker).
Kushoto ni Daktari Bingwa na Magonjwa ya Moyo Peter Kisenge. Tangu
kuanza kwa kambi hiyo mwanzoni wa juma hili jumla ya wagonjwa 20
wameshapatiwa matibabu kati ya hao nane wameshawekewa Pacemaker na
wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na kesho.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Peter Kisenge akiwaonyesha waandishi wa Habari jina la Dkt. Mathew
Sackett wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini Marekani
lilivyoandika katika nguo yake wakati wa mkutano baina yao uliozungumzia
kambi maalum ya matibabu ya Moyo inayoendelea katika Taasisi hiyo kwa
wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana na hivyo kuwekewa
kifaa maalum cha kuyarekebisha ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu
Pacemaker) .
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Tulizo Shemu na mwenzake kutoka Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini
Marekani Mathew Sackett wakimwekea mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha
mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa
hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo yao ya moyo yako chini sana. Tangu
kuanza kwa kambi maalum ya matibabu ya moyo jumla ya wagonjwa nane
wameshawekewa Pacemaker na wengine wanne wanatarajia kuwekewa leo na
kesho.
Wataalamu
wa Magonjwa ya Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na
wenzao wa Taasisi ya Madaktari Afrika ya Nchini Marekani wakimwekea
mgonjwa kifaa maalum cha kurekebisha mapigo ya moyo ili yawe sawa (kwa
jina la kitaalamu Pacemaker) kifaa hicho huwekewa wagonjwa ambao mapigo
yao ya moyo yako chini sana.
Picha na JKCI
SHARE
No comments:
Post a Comment