Muhubiri
wa kimataifa ‘Mama Afrika’ Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano
la kitaifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste
Church Makuburi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma, akifundisha katika kongamano hilo.
Mwenyekiti
wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith
Pentekoste Church, Dk. David Mwasota akizungumza katika kongamano hilo.
Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa waaminifu katika kila jambo.
Mafundisho yakiendelea.
Usikivu katika kongamano hilo
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Maaskofu wakiwa katika maombi.
Maombi yakiendelea.
Maombi yakifanyika.
Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria akitoa zawadi ya vitabu kwa maaskofu.
Maaskofu wakiwa kwenye kongamano hilo.
Na Dotto Mwaibale
VIONGOZI
wa dini wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kumsaidia Rais Dk. John
Magufuli kuliletea taifa maendeleo na kuondokana na umaskini nchini.
Mwito
huo umetolewa na muhubiri wa kimataifa ‘Mama Afrika’ Dk.Nicku Kyungu
wakati akihubiri katika kongamano la kimataifa la viongozi wa dini
lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es
Salaam leo.
Alisema
viongozi wa dini waliopo katika makanisa wanataaluma mbalimbali hivyo
mbali ya kuhubiri neno la mungu wanapaswa kutumia taaluma walizonazo
kumsaidia Rais katika maendeleo ya nchi jambo litakalosaidia nchi
kuondokana na umaskini na adui ujinga.
Dk.Kyungu alisema katika imani Tanzania sasa imetoka katika uchanga na sasa inakwenda mbele na hilo ni jambo la kujivunia.
Alisema
nchi ya Tanzania imebarikiwa tangu uongozi wa baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na
sasa Dk. John Magufuli.
“Ili ni
jambo la kujivunia kwa nchi kuwa na amani tangu wakati huo hadi leo hii
na ndio maana tumeona ni vizuri tukafanya maombi ya shukrani ya
kuliombea taifa na Rais wetu yatakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Uhurua
jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi” alisema Dk. Kyungu.
Dk.Kyungu
alisema kauli alioianzisha Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu ipo katika
biblia hivyo ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi kama mungu
alivyomuagiza adamu pale bustani ya hedeni.
Katika
kongamano hilo ambalo litakwisha kesho viongozi mbalimbali wa dini na
maaskofu kutoka ndani na nje ya nchi walipata fursa ya kuhubiri ambapo
Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa
waaminifu katika kila jambo.
Mchungaji
Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kutoka
mkoani Dodoma alisema kanisa hivi sasa limeingiliwa na magonjwa likiwemo
la waumini kuwanenea mabaya viongozi wao.
Maombi hayo ya shukrani kitaifa yatakayofanyika Jumamosi yameandaliwa Igo Africa for Jesus na Makanisa na Huduma za Tanzania
Maombi hayo ya shukrani kitaifa yatakayofanyika Jumamosi yameandaliwa Igo Africa for Jesus na Makanisa na Huduma za Tanzania
SHARE
No comments:
Post a Comment