Maelezo hayo ambayo Malima na dereva wake wamekana, yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage na Wakili wa Serikali, Ester Martin.
Malima na Ramadhani walikubali maelezo yao binafsi… siku ya tukio walikuwepo Masaki, kukamatwa na kushtakiwa pamoja na kuyakana mashtaka yote yanayowakabili ambapo kesi imeahirishwa hadi August 9 mwaka huu.
Katika kesi hiyo, Malima anadaiwa kuwa Mei 15, 2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi alimzuia Ofisa wa Polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali ambapo anadaiwa kumzuia Afisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.
Kwa upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed anakabiliwa na shtaka la kumshambulia Mwita Joseph ambaye ilidaiwa kuwa Mei 15, 2017 eneo la Masaki katika Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa Ramadhani akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni Afisa Oparesheni wa Kampuni ya Priscane Business Enterprises wakati anamkamata kwa kuegesha vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia na kumsababishia maumivu.
SHARE
No comments:
Post a Comment