Mkapa
alisema moyo wa kujitoa na kuwatumikia wananchi alionao Rais Magufuli
ndiyo chachu iliyomsukuma kumwamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa
Ujenzi kisha waziri kamili.
Rais
wa tatu Mkapa aliyasema hayo jana wakati wa sherehe ya makabidhiano ya
nyumba 50 za watumishi wa afya kwa mikoa ya Geita, Simiyu na Kagera
zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation kwa kushirikiana na Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
"Mimi
ninawashukuru zaidi nyie kwa kutambua nguvu zake, utawala wake, hali
yake, upeo wake, moyo wake wa kujitoa na kutumikia, na ndivyo
vilivyonivutia kumteua kuwa naibu waziri hadi kumpa uwaziri kamili,"
alisema Mkapa.
Alisema
mafanikio yanayopatikana sasa katika sekta ya afya ni juhudi za Rais
Magufuli hivyo anapaswa kupongezwa kwa asilimia mia moja.
"Kafanya kazi nzuri, na ataendelea kufanya kazi nzuri," alisema Mkapa. "Mafanikio haya yote ni katika sekta moja tu ya afya."
"Inatunza uaminifu wake, mnastahili kutoa kiongozi wa nchi nzima, tumshukuru Mungu kwa kutupa kijana huyu."
Miongoni
mwa mafanikio ya Rais Magufuli katika sekta ya afya, Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema jana,
ni ongezeko kubwa la bajeti ya wizara yake kwa miaka miwili iliyopita na
upatikanaji wa dawa kutarajiwa kuwa asilimia 90 na 100 kuanzia mwaka
huu wa fedha.
Waziri
Ummy ambaye Rais Magufuli alimsifu kwa kuwa mchapakazi hodari, alisema
hatua hiyo inatokana na MSD kutiii maagizo ya mkuu wa nchi huyo kuitaka
serikali iagize dawa kutoka kwa wazalishaji bila kupitia kwa dalali.
KAMPENI 1995
Kwa
upande wake, Rais Magufuli alisema anamshukuru Mkapa kwa kumpiga
kampeni mwaka 1995 wakati anagombea nafasi ya Ubunge wa Chato.
Alisema
wakati anagombea Ubunge, Mkapa wakati huo alikuwa anawania nafasi ya
Urais na alimnadi kwa wananchi wa Chato kuwa anafaa na hatimaye
alichaguliwa.
"Nakumbuka
mwaka 1995 ulipokuja ulikuwa umevaa viatu vyekundu... ulisimama pale
(akionesha sehemu ya uwanjani) na ukaniita jukwaani, ukanishika mkono na
kuniombea kura kwa wananchi wa Chato... asante sana," alisema Rais
Magufuli.
Aidha,
Magufuli alisema anamshukuru Rais mstaafu wa nne, Jakaya Kikwete kwa
kumwamini na kumteu kuwa Waziri katika wizara mbalimbali.
Rais
Magufuli aliishukuru Taasisi ya Mkapa Foundation kwa jitihada zake za
kujenga nyumba hizo kwa ajili ya watumishi wa afya, na kwamba taasisi
zingine ziige mfano huo.
"Mkapa
Foundation wameshatoa ajira zaidi ya 900 kwa madaktari, pia
wameshajenga nyumba zaidi ya 400," alisema Rais Magufuli. "Hayo ndiyo
maendeleo tunayoyataka, siyo zile taasisi zinaopigia debe wanafunzi
kuzaa."
Alisema
serikali imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka huu kutoka Sh.
bilioni 31 hadi Sh. bilioni 200 huku akiwataka wakuu wa mikoa, wilaya na
halmashauri kutumia vizuri pesa za kununulia dawa pindi
watakapopelekewa.
Kati ya nyumba hizo, 20 zimejengwa katika mikoa ya Geita, nyumba 20 katika mkoa wa Simiyu na nyumba 10 katika mkoa wa Kagera.
SHARE
No comments:
Post a Comment