SERIKALI imetangaza neema kwa
halmashauri zote nchini ikisisitiza kuwa watumishi watapandishwa vyeo na
ajira mpya zitatolewa kujaza nafasi za wote waliogundulika kuwa na
vyeti feki.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alisema
hayo jana jijini Dar es Salaam alipokutana na watumishi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Temeke kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema sasa serikali imepanga kutoa
ajira maalumu kwa kila halmashauri ili kujaza nafasi za watumishi
walioondolewa kazini baada ya kubainika kugushi vyeti pamoja na wengine
waliokuwa na vyeti feki.
“Nikianzia na Halmashauri ya Temeke,
niwahakikishie kuwa tatizo la watumishi litapungua na pia kwenye kila
manispaa iliyoondokewa na wafanyakazi kwa sababu ya vyeti feki, watapewa
idadi ileile ya watu ili waweze kujaza nafasi zao na hivyo, kuziba
mapungufu waliyoyaacha,” alisema Waziri Kairuki. Alisema zaidi ya
watumishi 133,000 wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke watapandishwa
vyeo katika kipindi cha Mwaka wa Fedha wa 2017/18.
Chanzo-Habarileo
SHARE
No comments:
Post a Comment