POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu tisa kwa tuhuma tofauti
akiwemo mkazi wa Kijiji cha Chingholwe, Kata ta Chanjale wilayani Gairo,
Bahati Malima kwa kumuua mkewe, Janet Sajilo (35) kwa kuchoma na kitu
chenye ncha kali sehemu ya kifuani na kufariki dunia papo hapo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei alisema jana kuwa mauaji hayo
yalifanyika juzi saa sita eneo la Kijiji cha Chingholwe, Kata ya
Chanjale, Tarafa ya Nongwe. Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo
ilidaiwa ni wivu wa mapenzi.
Alisema baada ya mtuhumiwa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali
kifuani, alifariki dunia papo hapo baada ya kuvuja damu nyingi.
Hata hivyo, alisema chanzo halisi kilichosababisha mume huyo kuchukua
uamuzi wa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani,
hakijafahamika na uchunguzi zaidi unaendelea na hatua za kumfikisha
mtuhumiwa mahakamani zitafuatwa.
Aidha, Haji Athuman (28) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Makambako,
Mkoa wa Njombe anashikiliwa na Polisi akiwa na simu aina mbalimbali
zipatazo 748. Simu hizo ni Tecno, Itel na Ditel pamoja na betri za simu
650 na chaja za simu 830.
IMEANDIKWA NA JOHN NDITI - HABARILEO MOROGORO
SHARE
No comments:
Post a Comment