Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Tarime Moses Misiwa Yomami akiongea katika baraza la Madiwani baada ya kupewa Hati safi ambapo ameomba kamati ya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua kali na kukamatwa kwa madiwani
wanao chochea Migogoro ya Mipaka katika Maeneo yao bila kuangalia chama.
"Kuna madiwani wengine wanadanganya wanachi wao kuwa wakiwachagua wataweza kupanua maeneo na kubadili mipaka jambo ambalo ni ndoto hivyo suala hilolinaweza kuchochea Migogoro na kuweza kuzua hatari kama kuna diwani wa hivyo bila kujali itikadi za vyama si CHADEMA wala CCM wakamatwe"
alisema Yomami.
SHARE
No comments:
Post a Comment