TRA

TRA

Wednesday, July 19, 2017

WANAFUNZI WAJISHINDIA MAMILION SHINDANO LA UWEKEZAJI DSE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Benson Mcharo amejinyakulia zawadi ya kiasi cha Sh. Milioni 2, baada ya kuibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha shindano la uwekezaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na shule za sekondari nchini, lilioandaliwa na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). 
Mcharo amekuwa mshindi upande wa wanafunzi wa vyuo vikuu, wakati Irene David kutoka Shule ya Sekondari ya Scolastica kutoka mkoani Moshi akijinyakulia zawadi ya milioni 1, baada ya kuibuka kidedea kwa upande wa wanafunzi wa shule za sekondari.
Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya ugawaji tuzo hizo,Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Tanzania (NEEC), Beng’i Issa ameipongeza DSE kwa kuandaa shindano hilo kwa kuwa linasaidia kutoa elimu ya masuala ya uwekezaji kwa wanafunzi nchini.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi za pesa walizozawadiwa, Mcharo amesema hakutarajia kuwa mshindi kwani shindano hilo lilikuwa na ushindani mkali na kwamba haikuwa jambo jepesi kuibuka kinara
“Nimefurahi sana kushinda, lakini shindano hili halikuwa rahisi sababu nilishiriki wakati nikiwa masomoni, na kupelekea kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja yenye kuhitaji utulivu wa akili,” amesema.
Naye Irene amesema amefurahi kupokea tuzo hiyo, na kwamba ataendelea kufanya uwekezaji kwenye soko hilo kwa ajili ya kujiingizia kipato pamoja na kupata elimu ya ziada ya kuwa mchumi bora hapo baadae.
Aidha, mshindi wa pili kwa upande wa vyuo vikuu ni Frank Johnson aliyejishindia mil. 1.5 kutoa Chuo cha Ardhi, wakati wa tatu akiwa ni Charles Msongwe (laki tano) kutoka SUA, huku nafasi ya nne ikichukuliwa na Omega Emanuel (laki tatu)kutoka SUA.

Kwa upande wa shule za Sekondari, nafasi ya pili ilichukuliwa na Christopher Ngonyani (Laki 6) kutoka Kibaha Boys, wakati wa tatu akiwa ni Emanuel Mwenda (Laki 4) kutoka Kibaha Boys.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger