Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji Nchini, liko katika mkakati wa kuingia
ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika shughuli zake za kukabiliana na
majanga ya moto ikiwa ni juhudi zake katika kuyafikia maeneo mengi
nchini.
Akizungumza
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dar es
salaam, Balozi wa Kuwait Nchini, Jasem Al-Najem, alisema serikali ya
Kuwait ipo tayari kubadilishana mafunzo na kutoa msaada wa vifaa kwa
Jeshi hilo.
“Ni
vema tukatengeneza mpango ambao wataalam wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji kutoka nchini Tanzania wataweza kubadilishana uzoefu na
wataalamu kutoka nchini Kuwait kwa ajili ya kujifunza mbinu mbalimbali
za kukabiliana na majanga pindi yanapotokea, ’’ Alisema Balozi huyo.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji, Thobias Andengenye alimshukuru kwa kumtembelea na kusema kuwa
ujio wa balozi huyo, umefungua ukurasa mpya kwa upande wa misaada na
mafunzo kwa Askari wa Jeshi hilo, kwani watapata fursa ya kubadilishana
uzoefu na kuongeza tija kwa Jeshi lake.
“Tutapata
nafasi ya kubadilishana uzoefu na kupata mafunzo kutoka Nchi ya Kuwait
na kuongeza ufanisi katika majukumu yetu ya kila siku, lengo ikiwa ni
kukabiliana na majanga mbalimbali yakiwemo ya moto,’’ alisema Kamishna
Jenerali.
Katika
kikao hicho Balozi wa Kuwait, Nasem Al-Najem alipokea taarifa ya
changamoto zinazolikabili jeshi hilo ikiwemo uhaba wa vitendea kazi huku
akiahidi kuzifanyia kazi na akisisitiza mchakato wa kusaini makubaliano
ya hiari ukamilike kwani utakuwa msaada wa kutekeleza kwa haraka
program za mafunzo ya muda mfupi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-MAKAO MAKUU YA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,
akimkabidhi zawadi Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kushoto),
baada ya mazungumzo na Balozi huyo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi
hilo, jjini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo aliahidi
kushirikiana na Jeshi kubadilishana utaalamu katika masuala ya
kukabiliana na majanga mbalimbali. Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,
akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (Wakwanza kulia)
alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam leo. Katika
Kikao hicho Balozi huyo aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo
kubadilishana utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali. Wengine ni Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo. Picha na Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akizungumza wakati wa kikao na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye
(katikati) na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo, alipotembelea Makao
Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam leo. Katika Kikao hicho Balozi huyo
aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika
masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye,
akiongozana na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem (kulia)
alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es Salaam
leo kwa mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati ya Majeshi ya nchi
hizo kubadilishana Utaalamu katika masuala ya kukabiliana na majanga
mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Balozi
wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji wakati alipowasili Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini
Dar es Salaam leo kwa mazungumzo na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo,
Thobias Andengenye(hayupo pichani). Katika Kikao hicho Balozi huyo
aliahidi kushirikiana na Jeshi hilo kubadilishana utaalamu katika
masuala ya kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto
na Uokoaji
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, akiwa
katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem
(katikati) baada ya kikao cha mazungumzo yaliyohusisha ushirikiano kati
ya Majeshi ya nchi hizo katika kubadilishana Utaalamu katika masuala ya
kukabiliana na majanga mbalimbali.Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
SHARE
No comments:
Post a Comment