Ofisa Uhusiano wa BANK OF AFRICA
tawi la Tandika, Beatrice Richard akimkabidhi zawadi ya (Tyre
Cover), Kevin Kihega kutoka mkoani Iringa aliyetembelea banda la
benki hiyo lililopo Namba 85 Sabasaba Hall katika maonyesho ya biashara
ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere
Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
O
Ofisa Uhusiano wa BANK OF AFRICA
tawi la Tandika, Beatrice Richard akihojiwa na mwandishi wa habari
wa Radio EFM aliyetembelea katika banda hilo, kushoto ni Muganyizi
Bisheko Muganyizi Bisheko Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo BANK OF
AFRICA.
Ofisa Uhusiano wa BANK OF AFRICA
tawi la Tandika, Beatrice Richard. Kulia Muganyizi Bisheko
Meneja Masoko/ Utafiti Maendeleo wa BANK OF AFRICA na katikati ni Emmy
Addie wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao.
Hapa wakifurahia jambo katika banda lao.
………………………………………………………………………
Muganyizi Bisheko Meneja
Masoko/ Utafiti Maendeleo BANK OF AFRICA amewakaribisha wananchi
kutembelea banda la maonyesho la benki hiyo lililopo namba 85 katika
ukumbi wa Sabasaba Hall viwanja vya J.K.Nyerere ili kupata taarifa
mbalimbali kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo yenye matawi kadhaa
jijini Dar es salaam na mikoani nchini Tanzania.
Akizungumza na Mtandao wa
Fullshangweblog katika maonyesho hayo Bw. Muganyizi amewakaribisha
wananchi kutembelea banda lao na matawi yake mbalimbali yaliyopo nchini
ili kujipatia huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na benki ya
BANK OF AFRICA ili kujikwamua kiuchumi na kuwezesha maendeleo katika
biashara zao.
Bw. Muganyizi amesema benki hiyo
inatoa huduma mbalimbali ambazo ni Mikopo ya Uwekezaji katika Nishati
Mbadala / Ufanisi wa Nishati, Ukodishaji wa Mitambo ya Uzalishaji mali
(Lease Finance) Ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu , Mikopo Midogo na ya
Kati na Huduma mbalimbali za akaunti na huduma za kibenki kwa njia ya
Kielektroniki
Bw. Muganyizi Bisheko Meneja
Masoko/ Utafiti Maendeleo wa benki hiyo amewakaribisha wananchi wote
katika banda lao ili kupata maelezo ya huduma mbalimbali zinazotolewa na
benki hiyo, Ameongeza kwamba wao kama BANK OF AFRICA wanayo furaha
kubwa kutumia fursa hii ya maonyesho ya Sabasaba wakiwa wanasherehekea
miaka kumi ya benki hiyo kwepo kwake nchini Tanzania
SHARE
No comments:
Post a Comment