Ofisa Mauzo wa Shirika la Bima la
Taifa, Vicent Rogath akipokea fedha kutoka kwa Askari wa Usalama
Barabarani Afande Kudra Mbura baada ya kukata bima ya magari yake
mawili kwa shirika hilo la taifa la Bima kwenye viwanja vya maonyesho ya
biashara ya Sabasaba yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J. K.
Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam kila mwaka kuanzia mwezi
wa saba, Maonyesho hayo yanaandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
ya Nje (TANTRADE) kushoto ni Afisa wa Bima Bi. Janeth Kalinga.
Ofisa Mwandamizi wa Bima,
Jumanne Nyamgunda akitoa maelezo kwa wananchi waliofika kwenye banda la
shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika
hilo katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya
Mwalimu JK. Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam
Ofisa Mwandamizi wa Bima,
Jumanne Nyamgunda akitoa maelezo kwa Dk. Ramesh Shah aliyekuwa
Jaji Mkuu wa Kamati ya Miss Tanzania wakati alipotembelea banda la
shirika hilo.
Wafanyakazi wa Shirika la Bima la
Taifa NIC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao lililopo
kwenye banda kuu la Wizara ya Fedha na Mipango.
Wafanyakazi wa Shirika la Bima la
Taifa NIC wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao lililopo
kwenye banda kuu la Wizara ya Fedha na Mipango.
SHARE
No comments:
Post a Comment