Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya
mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudani Kusini, Jenerali
Taban Deng Gai ambapo mazungumzo yao yalihusu kuendelea kudumisha
uhusiano baina ya nchi hizi mbili.
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati
mkutano wa 29 wa wakuu wa nchi na serikali wa Umoja wa Afrika, jijini
Addis Ababa ukihitimishwa.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
SHARE
No comments:
Post a Comment