Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme amefanya ukaguzi
kwenye vituo vya mafuta ili kuona kama wafanyabiashara ya kuuza mafuta
wanafuata sheria na taratibu za utoaji risiti na ulipaji kodi kwa
kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye
pampu au mita ya mafuta.
Katika
ziara hiyo Kati ya vituo 9 alivyovitembelea amegundua kituo kimoja tu
ndiyo kinafuata sheria na kuchukua hatua ya kuvifungia vituo nane.
Kazi hiyo imefanyika kwa kushirikiana na maafisa wa TRA Dodoma Mjini. Tunatekeleza kwa Hapa Kazi Tu, Lipa kodi kwa Maendeleo ya Taifa letu.
Pichani
kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh.Christina Mndeme
akishirikiana na Ofisa wa TRA kukifungia moja ya kituo cha mafuta mkoani
humo kilichobainika kutofuata sheria na taratibu za utoaji risiti na
ulipaji kodi kwa
kufunga mashine sahihi ya utoaji risiti iliyofungwa moja kwa moja kwenye
pampu au mita ya mafuta.
Wasimamizi wa kituo wakipewa maelekezo baada ya kituo chao cha mafuta kufungiwa
SHARE
No comments:
Post a Comment