Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medard Kalemani amepiga marufuku uagizaji wa nguzo za
umeme, nyaya na transfoma nje ya nchi na kuliagiza Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) kuhakikisha kuwa linanunua vifaa husika kutoka kwa
wazalishaji wa ndani. Dk. Kalemani aliyasema hayo wakati wa kikao
chake na watendaji wa TANESCO, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na
wazalishaji wa nguzo za umeme, transfoma na nyaya za umeme
kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es
Salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment