TRA

TRA

Sunday, July 9, 2017

Halotel yazindua vifurushi vipya vya shilingi 100

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imezindua rasmi huduma mpya yenye gharama nafuu zaidi itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kuwasiliana kwa kujiunga na vifurushi kwa kuanzia Shilingi 100, itakayowawezesha kupata dakika za kuongea usiku mzzima bure pamoja na kupata SMS na vifurushi vya intaneti vilivyopewa jina la CHIPSI BANDO.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo iliyofanyika katika banda la kampuni hiyo lililoko katika maonyesho ya 41 ya saba saba yanayoendelea, Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Stella Pius, Amesema kuwa lengo l kuanzisha huduma hiyo ni kuwawezesha Watanzania kuweza kumudu gharama za mawasiliano na kuona thamani ya kila salio wanaokuwa nalo kwenye simu zao.
"Tunatambua hitaji la mawasiliano rahisi miongoni mwa watanzania, hususan wateja wa Halotel ndio maana tumekuja na bando hili la kipekee litakalo wawezesha wateja wetu kuweza kuongea au kupata vifurushi vya intaneti kwa shilingi mia tu, ikiwa ni pamoja na kupata dakika za kuongea usiku mzima kwa shilingi 100 tu. Alisema Pius na Kuongeza
Mteja wa halotel anaweza kujiunga kwa kuanzia lisaa limoja  kwa Tsh. 100 na kuweza kupata: Dakika  za kwenda mitandao ya Halotel kwenda Halotel sekunde 200." Alisema na kuongeza kuwa "kwa Tsh 100, kwa lisaa limoja mteja anaweza kupata dakika za kwenda mitandao mingine, sekunde 100, huku pia kwa Tsh. 100 hiyo hiyo, mteja kwa lisaa limoja, anaweza kupata huduma ya data ambayo ni MB 25". 
Pius alihitimisha kwa kubainisha kwamba kwa kiasi hicho hicho cha shilingi 100, mteja wa halotel anaweza kupata dakika za kuongea Halotel kwenda Halotel bila kikomo, kuanzia saa sita usiku mpaka saa 12 asubuhi.
“Mteja anaweza kujiunga kwa kupiga *148*66#. Ambapo atapata  orodha ya huduma atakayopenda kati ya hizo. Ambapo anaweza kuchagua huduma namba mbili katika orodh na atapata Chipsi bando na kuweza kujiunga. Hii ni kwa wateja wote wa mtandap wa Halotel popote pale walipo” alisema.

Meneja Mawasiliano wa Halotel, Hindu Kanyamala akizungumza na baadhi ya wateja waliotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo, Katika maonyesho ya 41 ya sabasaba katika viwanja vya mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Kampuni hiyo imezindua vifurushi kwa wateja wa mtandao huo nchi nzima kuzungumza kwa shilingi 100 tu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger