TRA

TRA

Monday, July 17, 2017

JAMAL MALINZI NA MWESIGWA MAMBO BADO MAGUMU

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerudishwa rumande kwa mara nyingine kutokana na upelelezi  wa kesi yao kutokamilika hivyo wamerudishwa tena Mahakamani Julai 31 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.

Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea hadi  sasa.

Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger