Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye
akisalimiana na Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa
Iringa, mara baada ya kuwasili katika sherehe za makabidhiano ya gari la
kuzimia moto lililotolewa na Mdau Ndugu, Zakaria Hanspoppe kwenye kituo
cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani humo mapema jana asubuhi. (Picha
na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Askari
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakitoa salamu ya heshima kwa Mgeni
rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza, ambaye pia ni mwenyekiti
wa kamati ya vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo. (Picha na Jeshi
la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi katika
shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto akisalimiana na
Kamishna Jenerali wa Jeshi la ZImamoto na Uokoaji mara baada ya kuwasili
kituoni hapo mapema leo asubuhi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji)
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akisaini
kitabu cha wageni ambaye ameketi meza kuu katikati. (Picha na Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji)
Mdau
Ndugu Zacharia Hanspoppe (wa kwanza kushoto) ambaye ndiye aliyetoa
msaada wa gari la kuzimia moto kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akitoa
pongezi kwa Viongozi wa Jeshi hilo kwa jitihada wanazofanya katika
kukabiliana na majanga ya moto, mafuriko, ajali za barabarani na majanga
mengine. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza ambaye ni Mgeni rasmi akikata utepe
ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi gari la kuzimia moto kwa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, tukio ambalo limeshuhudiwa na Kamaishna Jenerali wa
Jeshi hilo, Viongozi mbalimbali wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani
humo, Mdau aliyetoa msaada huo Ndugu, Zacharia Hanspoppe, Maafisa na
Askari wa Jeshi hilo pamoja na wananchi. (Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji)
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji akionesha funguo ya gari hilo
mara baada ya tukio la kukata utepe na kukabidhiwa rasmi na Mkuu wa Mkoa
Bi. Amina Masenza ambaye alikuwa ni Mgeni rasmi katika makabidhiano
hayo. (Picha na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza mwenye kitambaa cheupe katikati,
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wa
kwanza mbele, Mdau ndugu Zachalia Hanspope wa pili kutoka kushoto,
pamoja na Viongozi wa kamati ya vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani
Iringa wakifurahi tukio la makabidhiano. (Picha na Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji)
Gari
lililokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza kwa Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoro na Uokoaji Thobias Andengenye. (Picha na
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza (kushoto) akiagana na Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye (kulia) mara
baada ya kuhitimisha shughuli ya makabidhiano ya gari la kuzimia moto
lililotolewa msaada na mdau Ndugu Zacharia Hanspoppe. (Picha na Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji).
SHARE
No comments:
Post a Comment