TRA

TRA

Tuesday, July 25, 2017

KAIMU MENEJA MKUU WA BANDARI YA KIGOMA AKANUSHA MADAI JUU YA KUTOKULIPWA WANANCHI 1228 WA ENEO KATOSHO

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za
Kigoma, Moris Mchindiuza  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika 
kikao cha menejimenti
kilichofanyikia katika majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo hawajalipwa fedha zao. Kushoto ni Meneja wa
Mawasiliano TPA,  Janeth Ruzangi.

 PRO wa TPA Tanga Moni
Jarufu akifuatilia mkutano huo
 Waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia matukio
 Waandishi wa habari
wakiwa kazini kuchukua stori
KAIMU
Meneja Mkuu wa Bandari za Kigoma, Moris Mchindiuza (kushoto) akimpa
ufafanuzi mwandishi wa gazeti la Dail News Mkoani Tanga, Amina
Kingazi.
KAIMU Meneja Mkuu wa Bandari za
Kigoma, Moris Mchindiuza amekanusha madai yanayoenezwa juu ya
kutokulipwa wananchi 1228 wa eneo la Katosho katika Manispaa hiyo kwa
ajili ya ujenzi wa mradi wa bandari kavu ambapo kiasi cha shilingi
Bilioni 12 zimetengwa kwa ajili ya gharama za fidia.
Hayo ameyazungumza jana Jijini
Tanga alipokuwepo kwenye kikao cha menejimenti kilichofanyikia katika
majengo ya bandari ya Tanga na kueleza kuwa zipo taarifa za upotoshwaji
zinazotolewa kuwa wananchi wanaostahili kulipwa ili kupisha mradi huo
hawajalipwa fedha zao.

Aidha alisema jumla ya hekari 158 ndizo zilizochukuliwa na mamlaka ya
bandari(TPA) kwa ajili ya mradi huo huku wananchi 1196 kati 1228 tayari
wamekwisha lipwa fedha zao kama semehemu ya fidia za ardhi,mazao na
makazi jambo ambalo limefanyika kwa mujibu wa kisheria na ushirikishwaji
wa pande zote.
Mchindiuza alizidi kufafanua kuwa
kutokana na hatua hiyo wananchi 32 kati yao walishindwa kulipwa fidia
zao kutokana na kushindwa kuwakilisha akaunti zao katika Halmashauri ya
manispaa ya Mji wa Ujiji jambo ambalo linapotoshwa na baadhi ya vyombo
vya habari.
“Yapo malalamiko mengi ya
utaratibu wa ulipwaji wa fidia hizo kwa wananchi walioko katika maeneo
ya ya maradi lakini labda niseme kitu tayari tumekwisha walipa wananchi
1196 kati 1228 na waliobakia ni 32 tu na fedha zao zipo wapeleke akauti
zao tuweze kuwalipa”Alisema.

Alisema Mamlaka hiyo baada ya kukua kutokana na kuongezeka kwa shehena
mamlaka ilitafuta eneo kwa ajili ya kujenga mradi wa bandari kavu ambalo
litatumika kuhudumia nchi jirani za maziwa makuu kama DRC,Burundi na
Rwanda.

Taratibu za kupatikana kwa eneo hilo ambalo lilikuwa mali ya wananchi
katika eneo hilo la Katosho Mkoani humo zilifanyika kisheria na
kuishirikisha Halmashauri ya Mji huo ambao wao ndio wanaozijua kaya
zinazoishi katika maeneo hayo.
“Lengo letu la kuishirikisha
Halmashauri ya manispaa hiyo ni
kuhakikisha wanafanya tathmini ya kina dhidi ya wananchi hao na
tunatambua kuwa wanazitambua kaya zote zinazostahili kulipwa na hivi
ndivyo tulivyo fanya”Alisema.

Hata hivyo aliwataka wananchi hao kama wanamadai kuhusiana na kiwango
kidogo cha fidia wanaweza kufika katika mamlaka za sheria za ardhi na
kufuata mkondo wa sheria ili waweze kupata msaada wa kisheria
zaidi.
“Wananchi wasipotoshwe na
wajanja wajanja idadi ya wafidiwa
inatambuliwa na na kama kuna kitu hakijafuatwa wafuate sheria ili mkondo
huo uchukue maamuzi ya kisheria bila ya kuonea mtu na sisi kama
viongozi wa mamlaka tupo salama na kwa wale ambao hawajalipwa wafike na
vielelezo katika ofisi husika wachukue fedha zao.



Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi hao waache kupotoshwa na watu
wachache ambao hawataweza kuwasaidia kitu chochote jambo la msingi
kujenga ushirikiano katika miradi hiyo ya maendeleo ya
Taifa.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii
ya Tanga Raha

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger