Mtendaji Mkuu Wa Benki Ya Tpb,
Sabasaba Moshingi (Wa Pili Kushoto) Na Kaimu Mkurugenzi Wa Mfuko Wa
Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini Wakitiliana Saini Makubaliano Ya
Kutoa Mikopo Ya Kielimu Na Kuazia Maisha Kwa Wanachama Wa Zssf, Hafla
Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf Kilimani Mjini Zanzibar.
Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Afisa Mawasiliano Wa Benki Ya Tpb Bi. Chichi
Banda (Kushoto) Na Afisa Wa Sheria Wa Zssf Bw. Fadhil Mohammed (Kulia).
Afisa Mtendaji Mkuu Wa Benki Ya
Tpb Bw. Sabasaba Moshingi (Wa Tatu Kushoto) Na Kaimu Mkurugenzi Wa Mfuko
Wa Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini Wakikabidhiano Mikataba Ya
Utoaji Mikopo Ya Kielimu Na Kuanzia Maisha Kwa Wanachama Wa Zssf, Hafla
Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf Kilimani Mjini Zanzibar.
Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Wakurugenzi Na Maofisa Kutoka Benki Ya Tpb Na
Mfuko Wa Hidhafi Ya Jamii Zssf.
Makabidhiano Ya Mkataba Wa Makubaliano Baina Ya Benki Ya Tpb Na Zssf.
…………………………………………………………………….
BENKI ya TPB imetiliana
saini na Mfuko wa Hifadhi Zanzibar (ZSSF), kwa ajili ya mkopo wa
kujikimu na wa elimu ya juu kwa wananchama wa mfuko huo. Utiaji wa saini
ulifanyika jana na kwa upande wa TPB, Afisa Mtendaji Mkuu, Sabasaba
Moshingi aliiwakilisha benki yake na kwa ZSSF iliwakilishwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Mfuko huo, Makame Mwadini Silima.
Akizungumza mara baada
ya utiaji wa saini hiyo Moshingi, alisema huduma hiyo muhimu kwa
wafanyakazi ambao wanaanza maisha na wale ambao wanataka kuongeza elimu
na kuwataka wanachama wa Mfuko huo kuchangamkia fursa ya mikopo ili
kujiendeleza kimaisha.
Alisema kuwa benki yao itakuwa ikitoa mikopo kwa wanachama hao na baada ya muda watakuwa wakirjesha kwenye mishahara yao.
Alisema kuwa katika
huduma hiyo kila atakayekopa atakaywa riba ya asilimia 12 ya mkopo wake
ambayo aliielezea ni ndogo kulingana na aina ya riba ya mikopo mengine.
Alisema kuwa huduma hii
ya mkopo wa kujikimu na wa elimu ya juu imeanza Dar es Salaam kupitia
Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na GEPF na jana ZSSF walitiliana
mkataba baada ya kuona umuhimu wa kuwasaidia wanachama wao.
Kaimu Mkurugenzi wa
ZSSF, Mwadini alisema kuwa hatua hiyo mbali ya kuwawezesha wananchama
wao, itawasaidia kuongeza wanachama wapya kwa sasa wana wanachama zaidi
ya 70,000.
Alisema kuwa wamefanya
mambo mbalimbali ikiwamo kukabiliana na changamoto za wanachama wao na
kuboresha ustawi wa Wazanzibari na Watanzania.
SHARE
No comments:
Post a Comment