Makabidhiano
ya funguo yakiendelea baina ya Meneja wa Wakala wa majengo Mkoa wa
Mwanza, Yohana Mashausi na Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Kilimo
nchini, Francis Assenga, huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mwenye kofia
akishuhudia tukio hilo
Kaimu
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo kwa Wakulima nchini akiteta jambo na
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella mapema kabla ya makabidhiano hayo
kwenye eneo la tukio (Picha zote na Ofisi ya Mkuu wa mkoa)
Jengo hapa likifunguliwa tayari kukaguliwa na kukabidhiwa kwa wahusika.
Mwandishi
wa habari kutoka Magazeti ya serikali Nashonny Kennedy, akitaka
uafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Wakulima
nchini, wakati wa hafla ya Makabidhiano ya Benki hiyo.
(Picha na Atley Kuni- Mwanza)
……………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu,
Katika kutimiza ahadi ya Mhe.
Rais Dk. John Magufuli, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
imedhamiria kuwaneemesha wakulima wa Kanda ya Ziwa kwa kufungua Ofisi ya
Kwanza ya Kanda yenye lengo la kuwapatia mikopo yenye gharama nafuu
wakulima wa Kanda ya Ziwa.
Akizungumza wakati wa makadhiano
ya jengo litakalotumika kama Ofisi ya TADB Kanda ya Ziwa, Mkuu wa mkoa
wa Mwanza, Mhe. John Mongella alisema kuwa Benki ya Kilimo ikiwa ni
taasisi ya umma ina wajibu kusaidia juhudi za Serikali katika kuinua
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania hasa katika
kuchagiza mapinduzi na maendeleo katika Sekta ya Kilimo, ambayo inaajiri
zaidi ya asilimia 75 ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi nchini na pia
kutoa kiasi cha zaidi ya asilimia 65 cha mali ghafi kwa ajili ya
viwanda vya nchi.
“Uanzishwaji wa TADB unatokana na
Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji wenye tija kwenye maeneo yote ya
sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati ya Kilimo ili kuwezesha
upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa ni pamoja na
kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa mikopo
zaidi kwenye sekta ya Kilimo,” amesema.
Mhe. Mongella alisema kuwa Kanda
ya Ziwa ina utajiri mkubwa kwenye uzalishaji wa mazao ya chakula na
biashara ambayo ni mojawapo wa minyororo ya thamani ya mwanzo
inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao mbalimbali na
Benki ya Kilimo.
Aliongeza kuwa maendeleo ya sekta
ya kilimo inahitaji msaada mkubwa wa uwezeshwaji wa mikopo kutoka TADB
kwa kuzingatia kuwa ni chombo cha serikali kilichoanzishwa ili kusaidia
upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini
Tanzania.
“Kwa kutambua jukumu kubwa la
TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo
cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi
na kupunguza umaskini, Ofisi ya Mkoa wa Mwanza iliona kuna umuhimu wa
kuipatia Benki hii jengo hili iweze kuwafikia wakulima wa Kanda ya Ziwa
na maeneo ya jirani,” aliongeza.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga alisema Benki ya Kilimo
imedhamiria na kujizatiti kuhakikisha inachangia kwa kiasi kikubwa
katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa
kusaidia upatikanaji na utoaji wa fedha ikiwa ni pamoja sera nzuri
zitakazosaidia maendeleo ya kilimo nchini.
Bw. Assenga aliongeza kuwa TADB
imejipanga kutekeleza malengo ya Serikali katika kuanzisha Benki hiyo
ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha upatikanaji wa
mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika kilimo
nchini.
“Kanda ya Ziwa ni eneo la
kimkakati hivyo ujio wetu ni kutimiza dhamira ya dhati ya serikali
katika kutatua changamoto za ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha
mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini unachangiwa kwa kiasi
kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye
upande wa biashara za bidhaa; riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo; mikopo
ya muda mfupi; masharti magumu ya kukopa bila kuzingatia hali halisi ya
sekta ya kilimo na mazao ambayo inaathiriwa kwa kiasi kikubwa na
mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema.
Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo
imejipanga kushirikiana na Serikali, wabia wa kimkakati na wadau wengine
katika kuendeleza sekta ya kilimo, hasa kuboresha na kutekeleza na
juhudi zozote sera zinazohusiana na kuhisha ushiriki wa wananchi kwenye
mifumo ya kifedha.
SHARE
No comments:
Post a Comment