Beyonce hatimaye amesambaza picha ya kwanza aliyopiga na watoto wake pacha kuadhimisha mwezi mmoja tangu wazaliwe.
Msanii
huyo wa Marekani alithibitisha kwamba majina yao ni Sir Carter na Rumi
ambayo yalitolewa katika uvumi baada yeye na mumwe kuyatumia kama nembo
ya biashara.Picha hiyo inamuoyesha mama huyo mwenye umri wa miaka 35 na pacha hao wakiwa ndani ya shiti la rangi ya zambarau huku yeye mwenye akiwa amevalia vazi la rangi ya buluu.
- Beyonce atarajia kujifungua mapacha
- Beyonce Knowles ajifungua pacha
- Beyonce kufanya tamasha akiwa mjamzito
Beyonce aliandika: Sir Carter na Rumi wamefikisha mwezi mmoja leo huku akiweka emoji ya mikono ya maombi na mwanamke, mwanamume na watoto wawili.
Mbali na pacha hao ambao ni mvulana na msichana Beyonce na JAY-Z pia ni baba wa mtoto wa miaka mitano Blue Ivy.
Mtindo wa picha hiyo ambapo Beyonce amesimama katika bustani akiwa hana viatu mbele ya eneo lenye maua unafanana na picha aliyopiga akitangaza uja uzito wake katika mtandao huo.
Ulimwengu ulikuwa ukisubiri kwa hamu kuwaona watoto hao tangu vyombo vya habari viliporipoti kwamba mwimbaji huyo wa Lemonade alikuwa amejifungua mwezi uliopita.
Lakini hakuna kati yao aliyethibitisha pacha hao .
- Beyonce ashauriwa kupumzisha sauti yake
- Beyonce atawala tuzo za MTV Marekani
- Adele amempa Beyonce tuzo yake ya Grammy?
Haishangazi kwamba mashabiki walilazimika kusambaza maoni yao katika picha hiyo. DJ wa BBC radio One Clara Amfo aliandika katika Twitter: Soo extra and I love it.
SHARE
No comments:
Post a Comment