Bodi
ya Wadhamini ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
imewaachisha kazi wafanyakazi 12 waliokuwa wamesimamishwa kwa mwaka
mmoja sasa.
Wafanyakazi hao walisimamishwa kazi Julai 2016 kupisha uchunguzi kuhusu tuhuma za ubadhirifu na matumizi mabaya ya ofisi.
Taarifa
ya NSSF iliyotolewa leo Alhamisi (Julai 13) kupitia vyombo vya habari
walioachishwa kazi ni Yacob Kidula, aliyekuwa mkurugenzi wa mipango,
uwekezaji na miradi.
Wengine
na nafasi walizokuwa wakishikilia kwenye mabano ni Ludocick Mrosso
(mkurugenzi wa fedha), Chiku Matessa (mkurugenzi wa rasilimali watu na
utawala), Sadi Shemliwa (mkurugenzi wa udhibiti, hadhara na majanga),
Pauline Mtunda (mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za ndani).
Crescentius
Magori (mkurugenzi wa uendeshaji), Amina Abdallah (meneja utawala),
Abdallah Mselli (meneja wa uwekezaji), Mhandisi John Ndazi (meneja
miradi), Wakili Chedrick Komba (meneja kiongozi Mkoa wa Temeke) na
Ramadhani Nassibu (meneja mkuu usalama).
SHARE
No comments:
Post a Comment