Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akizungumza na wachezaji wa
timu za Kata za Nkiniziwa na Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa
michuano ya Kigwangalla Cup 2017, iliyofanyika kwenye viwanja vya shule
ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na timu ya Kata ya
Mzibaziba wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017,
iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo
zilitoka droo ya bao 1-1.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na wachezaji wa Kata ya
Nkiniziwa wakati wa ufunguzi rasmi wa michuano ya Kigwangalla Cup 2017,
iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingizi Nkiniziwa, timu hizo
zilitoka droo ya bao 1-1.
…………………………
Na Mwandishi Wetu
Mashindano ya mpira wa miguu kwa
timu za Kata zilizo ndani ya Jimbo la Nzega Vijijini maalufu kama
‘Kigwangalla Cup’ yamezinduliwa rasmi jioni ya Julai 27, 2017 huku
miamba 20 ikitarajiwa kuumana kumpata bingwa wa Jimbo hilo kwa mwaka
huu.
Awali akizungumza wakati wa
uzinduzi huo, Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi
Kigwangalla aliwataka wachezaji wote wanaoshiriki michuano hiyo kuwa na
nidhamu iliwaitumie michuano hiyo kama kipimo cha wao cha kuonesha
vipaji vyao ili waonekane ngazi za juu.
“Mpambane kweli kweli. Kila mmoja
wenu aoneshe uwezo wake wa kusakata kabumbu. Pia muzingatie nidhamu ya
hali ya juu kwani michezo inaleta umoja na amani, inaimalisha afya ya
miili yetu” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akuzungumza na wachezaji
katika ufunguzi wa michuano hiyo.
Dk. Kigwangalla pia alipata wasaha
wa kukagua timu zilizofungua rasmi michuano hiyo kati ya Mizibaziba
dhidi ya Nkiniziwa ambazo hadi kipyenga cha mwisho ziliweza kutoka droo
ya bao 1-1.
Dk. Kigwangalla alieleza kuwa,
jumla ya Kata 19 za jimbo lake hilo zimeweza kutoa timu ilikushiriki
michuano hiyo huku timu maalum ikiingizwa ambayo itajumuisha Madiwani
wote kutoka Kata hizo ili kufanya jumla ya timu 20.
Dk. Kigwangalla alizitaja baadhi
ya Kata zinazochuana kwenye michuano hiyo ni pamoja na Kata ya Puge,
Ndala, Nata, Sanzu,Lusu, Milambo Itobo, Magengati,Budushi, Nkiniziwa,
Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi.
Kata zingine ni Kata za Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
Awali kabla ya kuanza rasmi kwa
mchezo wa ufunguzi, Madiwani wa Kata zote waliweza kukabidhiwa baadhi ya
vifaa kwa timu zao sambamba na hilo wananchi waliweza kufurahia michezo
mbalimbali ikiwemo ile ya jadi hasa mchezo wa asili wa bao la
Kinyamwezi, kucheza drafti, kukimbiza kuku, michezo ya mbio kwa Wazee
huku mchezo wa mbio kwa watu wenye vitambi ukitia fola kwenye ufunguzi
huo, uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Nkiniziwa iliyopo
kwenye Kata hiyo ya Nkiniziwa.
SHARE
No comments:
Post a Comment