Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour
ameweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures iliyopo
katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika Manispaa ya
Shinyanga.
Amour ameweka jiwe la msingi katika shule hiyo ya Binafsi inayotoa elimu ya awali na msingi leo Jumanne Julai 11,2017.
Akisoma taarifa fupi kwa ki ngozi huyo,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Little Treasures,Paul Kiondo alisema mradi huo wa vyumba vine vya
madarasa na matundu nane ya vyoo umegharimu shilingi milioni 120.
“Jengo hili lenye kiwango na ubora wa hali ya juu ili kutoa mazingira
bora ya ufundishaji na ujifunzaji, lina uwezo wa kubeba wanafunzi
180Madarasa haya manne ni kati ya 15 yaliyopo katika shule hii,ujenzi
ulianza mwaka 2016 na umekamilika mwezi Juni 2017 ambapo shule imetumia
rasilimali zake za ndani”,alieleza Kiondo.
“Hivi sasa tupo katika mchakato wa kujenga shule ya sekondari ili
wahitimu wa shule hii watakaopenda waendelee na masomo ya sekondari hapa
hapa,lengo letu ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu kwa mujibu wa
matakwa na muongozo wa serikali yetu tukufu”,aliongeza Kiondo.
Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa , Amour Hamad Amour
alimpongeza mwekezaji aliyejenga shule hiyo kwa kuona umuhimu wa
kuwekeza katika elimu na kuongeza kuwa serikali inatambua jitihada nzuri
zinazofanywa na watu binafsi katika sekta ya elimu nchini.
"Serikali yetu inasisitiza viwanda,ili kufanikisha vizuri zaidi
tunahitaji wataalamu wa kuendesha viwanda hivyo,hivyo tunapaswa kuwapa
wanafunzi wetu elimu itakayowezesha kupata wasomi waliobobea katika
viwanda",alisema Amour.
"Naomba uongozi wa shule ushirikiane na serikali kuhakikisha watoto
wanapata elimu bora na elimu bora inategemea walimu bora,jukumu la
uongozi wa shule kuhakikisha kuwa walimu wanaojituma ipasavyo katika
ufundishaji",aliongeza Amour.
Mwandishi Mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika shule ya msingi Little Treasures.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour
akijiandaa kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little
Treasures leo Jumanne Julai 11,2017.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour
akikata utepe wakati wa kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi
Little Treasures.
Jiwe la Msingi la Shule ya Msingi Little Treasures limewekwa na kiongozi
wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Amour Hamad Amour.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures,Paul Kiondo akifungua
mlango ili kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour
(aliyevaa miwani) aingie ndani ya jengo hilo kuangalia vyumba vya
madarasa.Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour (kushoto)
akiwa katika moja ya madarasa ya jengo jipya la shule ya msingi Little
Treasures.
Muonekano wa jengo hilo jipya la shule ya msingi Little Treasures lenye vyumba vinne vya madarasa
Jengo jipya la shule ya msingi Little Treasures.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza katika shule ya Msingi Little Treasures
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Little Treasures wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour
akiwa jukwaani na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures.
Kushoto ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Geofrey
Mwangulumbi akifurahia jambo,anayefuatia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Little Treasures Paul Kiondo na Meneja wa shule ya Msingi Little
Treasures Mwita Nchagwa (wa tatu kushoto akipiga picha wanafunzi wake)
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour
akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo alisisitiza
wazazi na walezi kusomesha watoto wao kwani elimu ndiyo msingi wa maisha
yao.
Kulia ni Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa na
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures Paul Kiondo
wakifuatilia hotuba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka
2017,Amour Hamad Amour.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures.
Wanafunzi wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba wimbo mbele ya
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour
(kulia).
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakicheza wimbo mbele ya
kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakijiandaa kuushika mwenge wa uhuru.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakishika mwenge wa uhuru
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiendelea kuushika
mwenge wa uhuru.Kushoto Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little
Treasures,Paul Kiondo.
Mwenge wa uhuru ukiondolewa katika shule hiyo.
Gari linalobeba mwenge wa uhuru.Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa shule
za jirani na shule ya msingi Little Treasures wakiwa eneo la tukio.
Wanafunzi wakiendelea na shughuli zao baada ya mwenge wa uhuru kuondolewa shuleni hapo.
Wanafunzi wakiendelea na masomo.
Jengo la utawala katika shule ya Msingi Little Treasures.
Muonekano wa baadhi ya madarasa katika shule ya msingi Little Treasures.
Majengo yaliyopo katika shule ya msingi Little Treasures
Magari kwa ajili ya wanafunzi yakiwa shuleni muda wa masomo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
SHARE
No comments:
Post a Comment